Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2025

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA

Picha
  Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wametangaza kujiengua na Chama hicho kwa madai ya mpango wake wa kuendesha Oparasion ya Bila mageuzi hakuna uchaguzi Wanachama hao wamedai kuwa hatua hiyo inawanyima haki yao ya Msingi ya kuchagua na kuchaguliwa   Wakiongea na Waandishi wa Habari mjini  Kibondo mmoja wa Wajumbe wa Kamati tendaji na Katibu Msiaafu wa Chadema Wilaya ya Kibondo  Lenatus Richadi alikuwa wakwanza kutangaza kijiengua kwenye Chama hicho na kueleza kuwa hajawa na mpango wa kujiunga na chama kingine kwa sasa   Wanachama walioamua kujitenga na Chadema Wilaya ya Kibondo kwa sasa Idadi yao ni 40 na wanadai muda uliopo kufanya mageuzi na kurekebisha taratibu zingine ili chadema ikubali na iendelee uchaguzi 2025 ni mfupi sana hivyo haki zao watazikosa   ‘’ Kweli nakipenda Chama change kimenitoa mbali sana lakini utaratibu huu na misimamo iliyopo siwezi kuendelea...