Kibondo;Idadi kubwa ya Wakimbizi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma ni moja ya changamoto zinazoukabili mkoa huo ikiwa usalama mdogo kwa baadhi ya wenyeji, uharibifu wa miundo mbinu, na mazingira
Bruno Nkwabi Kaimu Mkuu wa Makazi James Mwangi ofisa Mazingira UNHCR Revocatus Nginila Mratibu Redeso Kibondo; Idadi kubwa ya Wakimbizi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma ni moja ya changamoto zinazoukabili mkoa huo ikiwa usalama mdogo kwa baadhi ya wenyeji, uharibifu wa miundo mbinu, na mazingira Wakimbizi hao walioko katika makambi ya Nyarugusu Kasulu, Mtendeli Kakonko na Nduta Kibondo, wanakadiliwa kufikia 270 ambapo uharibifu uko kwa kiwango cha juu huku uoto wa asili na vyanzo vya maji vikikauka hali ambayo inatishia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi Akiongea wiki iliyopita na Wakimbizi wa Kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo kaimu mkuu wa makazi wa kambi hiyo, Bruno Nkwabi amewataka kutunza mazingira na mali asili zote walizozikuta ambazo zinawasaidia hata wao ''Lazima mkumbuke wakati mnaingia kwenye maeneo haya mlikuta kila kitu kiko vizuri na mliweza kufurahia hivyo lazima mue...