Kibondo;Idadi kubwa ya Wakimbizi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma ni moja ya changamoto zinazoukabili mkoa huo ikiwa usalama mdogo kwa baadhi ya wenyeji, uharibifu wa miundo mbinu, na mazingira
Bruno Nkwabi Kaimu Mkuu wa Makazi |
James Mwangi ofisa Mazingira UNHCR |
Revocatus Nginila Mratibu Redeso |
Kibondo;Idadi kubwa ya Wakimbizi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma ni moja ya changamoto zinazoukabili mkoa huo ikiwa usalama mdogo kwa baadhi ya wenyeji, uharibifu wa miundo mbinu, na mazingira
Wakimbizi hao walioko katika makambi ya Nyarugusu Kasulu, Mtendeli Kakonko na Nduta Kibondo, wanakadiliwa kufikia 270 ambapo uharibifu uko kwa kiwango cha juu huku uoto wa asili na vyanzo vya maji vikikauka hali ambayo inatishia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi
Akiongea wiki iliyopita na Wakimbizi wa Kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo kaimu mkuu wa makazi wa kambi hiyo, Bruno Nkwabi amewataka kutunza mazingira na mali asili zote walizozikuta ambazo zinawasaidia hata wao
''Lazima mkumbuke wakati mnaingia kwenye maeneo haya mlikuta kila kitu kiko vizuri na mliweza kufurahia hivyo lazima muendeleze hali mliyoikuta kwa kutambua kuwa kila kitu kilitunzwa'' alisema Nkwabi
Kutokana na wingi wa Wakimbizi hao na maeneo wanayoishi baadhi yao Imana ilakiza Bosco na Janeviva Emmanuel walisema wamekuwa wakilazimika kutafuta nishati ya kupikia na wakiipata kwa shida kwa kuingia katika maeneo ya wenyeji
Kwa upande wake Mratibu wa shirika linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira katika Kambi za Nduta na Mtendeli la Redeso, Revocatus Nganila alisema changamoto iliyopo ni kutokana na serikali kutotenga maeneo maalum ya kupata nishati kama kuni kwa ajili ya matumizi
Aidha Nginila aliongeza kuwa wao shirika lenye dhamana lenye uhifadhi wa mazingira wamekuwa wakijitahidi kuielimisha jamii ya ya wakimbizi juu ya matumizi ya majiko banifu yanayotumia kuni chache na kuwataka kutokata miti mibichi bali iliyokauka ikiwa ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji
ofisa mazingira wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, James Mwangi akisema ipo haja ya kuweka mikakati maalum juu ya uhifadhi wa mazingira kwa wakimbizi na Wananchi wenyeji ili kufikia malengo yanayokusudiwa na kunusuru Vizazi vijavyo
,Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni