Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2025

Ukubwa wa Mpaka wa Mkoa wa Kigoma chanzo Njia za Panya nyingi na kuingiza Wageni haramu

Picha
  Toyi Silvesta Diwani Kata ya Gwanumpu Kakonko Kigoma akiongea na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhala Ukubwa wa Mpaka wa Mkoa wa Kigoma chanzo Njia za Panya nyingi na kuingiza Wageni haramu Kigoma;Kutokana na Mkoa wa   Kigoma   kuwa na   Mpaka mrefu sana kuliko Mikoa yote ya pembezoni huku vituo rasmi vya uhamiaji vikiwa mbali mkubwa   toka kituo kimoja hadi kingine   hatua inayodaiw a kupelekea   uwepo wa   njia za panya nyingi na wahamiaji haramu kupata ulaisi wa kuingia nchini jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Tanzania Mkoa huo unapakana na   Nchi za Burundi na Congo DRC upande wa Magharibi na nchi hizo zimekuwa zikikumbwa na matatizo ya usalama na kupelekea Raia wa   nchi   hizo kukimbia kutafuta sehemu salama Raia wa Nchi jirani wanadaia kuingia Tanzania kwa Vigezo vya kutafuta vibarua kupata Mkate katika maeneo vya Vijiji vya Mpakani Mkoani Kigoma na baadae ulazimika kuendelea kukaa Vijijini humo kinyume cha sheria z...

KUHITIMISHA UCHUKUAJI FOMU KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE JIMBOLA MUHAMBWE CCM

Picha
  rAPHAEL SUMAYE KATIBU CCM WILAYA YA KIBONDO Chama cha Mapinduzi Ccm kimehimisha zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania fafasi za Ubunge na Udiwani kamalilivyoanza June 28,2025 hadi leo julai 2,2025 kwa Wanachama wake kwa ajili ya uchaguzi Mkuu   kuwapata Madiwani,Wabunge na Rais unaotarajiwakufanyika octoba mwaka huu   Katika Jimbo la Muhambwe Kibondo Mkoani Kigoma,wamejitokeza Wananchama wa Ccm walioonyesha Nia ya kugombea ubunge   kuitia ccm idadi imetajwa ni 17   na wote wamerejesha fomu zao kwa wakati     Aidha Sumaye amesema baada ya hatua hiyoya awali   itaendelea michakato mingine ili kifikia malengo yanayokusudiwa huku Waliochukua fomu kugombea udiwani Kata zote   ikitajwa idadi ni    wanachama 96 na hakuna malalamiko yaliyojitokeza   kwa madai ya kutotendewa haki   Jimbo la Muhambwe linaundwa na   Vitongoji   420,Vijiji 50 na Kata 19 huku baadhi ya watia ambao ni Adrian Thoma A...

Mnyukano Ubunge Muhambwe

Picha
Jamal Abdlah Mwenyekiti Ccm Mkoa wa  Kigoma achukua Fomu  kugombea Ubunge Jimbo la Muhambwe   Frolence Samizi Mbunge Muhambwe anaetetea Kiti chake  achukua fomu ubunge Muhambwe Kuelekea uchaguzi Mkuu 2025,Wanachama wa   Chama cha Mapinduzi Ccm Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wameendelea kujitokeza   kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge   kwa ajili ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu   Baadhi ya wanachama hao mmoja wapo ni Mwenyekitiwa Ccm Mkoa wa Kigoma Jamali Abdalah ambaye   ametia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Muhambwe Kibondo kwa kuchukua Fomu kwenye ofisi za Ccm wilayani Kibondo   Frolence Samizi ambaye ni Mbunge anaeteteaKiti chake nae amechukua fom kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine tena huku wakifuatiwa na wanachama wengine Nduhilabusa Mapigano Katibu Jumhiya ya Wazazi Wilaya ya Kasulu,   Geradina Kabululu na wengine   Kwaupande wake Katibu w...

Iran yadai kupata hati nyeti za nyuklia za Israeli kupitia ujasusi

Picha
  Televisheni ya taifa ya Iran iliripoti Jumamosi kwamba Iran imepata hati nyeti za nyuklia za Israel kupitia "uvamizi mkubwa wa kijasusi." Ripoti hiyo haikutoa maelezo ya kina juu ya jinsi Iran ilipata ufikiaji wa hati hizo. Habari hiyo ilitangazwa kwa ufupi kwenye TV ya serikali kwamba "huduma za kijasusi za Iran zimepata taarifa na nyaraka za kimkakati na nyeti, ikiwa ni pamoja na maelfu ya nyaraka zinazohusiana na miradi na vifaa vyake vya nyuklia (Israeli)." Israel bado haijatoa maoni yoyote kuhusu dai hili la Iran. Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Tasnim, Waziri wa Ujasusi wa Iran Hojatoleslam Seyyed Esmail Khatib alisema kuwa "nyaraka za nyuklia za Israel zimehamishiwa Iran.

Israel yaishambulia Iran kwa makombora, yenyewe yaahidi kulipiza kisasi

Picha
  Taharuki imetanda mashariki ya kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel katika mji mkuu wa Iran, Tehran, Ijumaa asubuhi. Milipuko mikubwa ilisikika kote Tehran, huku Israel ikitangaza kuwa imelenga maeneo ya nyuklia na vituo vya kijeshi. Mashambulizi haya yanakuja wakati mvutano kati ya nchi hizo mbili umefikia kiwango cha juu kabisa kufuatia maendeleo ya haraka ya mpango wa nyuklia wa Tehran. Mashambulizi hayo pia yalipiga mji wa Kermanshah magharibi mwa Iran, ambapo wakazi walisema walisikia milipuko na kuona moshi mweusi ukipanda juu ya jiji. Haikubainika mara moja ni nini hasa kililengwa. Milipuko pia ilisikika karibu na mji wa Tabriz nchini Iran, ingawa hali halisi huko bado haijawa wazi.

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA

Picha
  Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wametangaza kujiengua na Chama hicho kwa madai ya mpango wake wa kuendesha Oparasion ya Bila mageuzi hakuna uchaguzi Wanachama hao wamedai kuwa hatua hiyo inawanyima haki yao ya Msingi ya kuchagua na kuchaguliwa   Wakiongea na Waandishi wa Habari mjini  Kibondo mmoja wa Wajumbe wa Kamati tendaji na Katibu Msiaafu wa Chadema Wilaya ya Kibondo  Lenatus Richadi alikuwa wakwanza kutangaza kijiengua kwenye Chama hicho na kueleza kuwa hajawa na mpango wa kujiunga na chama kingine kwa sasa   Wanachama walioamua kujitenga na Chadema Wilaya ya Kibondo kwa sasa Idadi yao ni 40 na wanadai muda uliopo kufanya mageuzi na kurekebisha taratibu zingine ili chadema ikubali na iendelee uchaguzi 2025 ni mfupi sana hivyo haki zao watazikosa   ‘’ Kweli nakipenda Chama change kimenitoa mbali sana lakini utaratibu huu na misimamo iliyopo siwezi kuendelea...

MIRADI YA MAJI THAMANI YA FEDHA IONEKANE

Picha
  Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko   Muhingo Mwemezi Kigoma Kutokana na serikali kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji Miundombinu   ya Maji, Wasimamizi wa Miradi hiyo wametakiwa kuahakikisha thamani ya fedha hizo inaonekana ili kuleta tija na kuondoa changamoto kwa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta Maji na kushindwa fanya shughuli za uzalishaji Kadri Miradi inavyoongezeka vivyo hivyo na migao ya Maji ipungue kwenye maeneo ya wananchi na huduma ziwe bora ikiwa ni pamoja na ankala halisi zinazotakiwa kulipwa na wananchi Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma Evance Malasa, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya Maji yaliyofanyika Kijiji cha Nyanzige kata ya Nyamtukuza ambapo amesema ni vema Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa wilayani humu kujitathimini na kufanya maboresho ya utoaji wa   huduma za Maji Maadhimisho hayo yameambatana na uwekaji jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi Mkubwa...

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Picha
    Muhingo Mwemezi Kibondo Baraza la Halmashauri ya Kibondo na Kikao cha ushauri cha Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma vimepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la Muhambwe kuwa majimbo mawili kwa kile kinachotajwa kuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi Daniel Ndalangavye ni Afisa uchaguzi halmashauri ya kibondo yeye katika taarifa yake anasema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa na Tume huru ya uchaguzi Tanzania ikiwa baadhi yake ni Idadi ya Watu, Ukubwa wa Eneona ukusanyaji wa ushuru na kodi huku akieleza kuwa kulingana na Jiografia ya eneo   wananchi wengi wamekuwa wakipata usumbufu kuifikia ofisi ya Mbunge kwa sasa kutokana na umbali hivyo Jimbo likigawanywa   Wabunge wa Majimbo hayo wataweza kuwahudumia wananchi kwa ufasaha zaidi Awali Jimbo la Muhambwe liliitwa Kibondo na mwaka 2010 likagwaanywa Majimbo mawili Buyungu Kakonko baadae kuitwa Muhambwe na sasa inapendekezwa Muhambwe kugawanywa tenda ambapo wajumbe wajumbe wa Baraza na Kika...

RUSHWA YANGONO BADO NICHANGAMOTO KWA WANAWAKE NA WASICHA KATIKA MASUALA YA MAENDELEO

Picha
Baadhi ya Wanawake walioshiriki maadhimisho siku ya Wanawake Duniani March8,2025 Hidaya Kimpwi Mkazi wa Buhigwe Aggripina Buyogela Mwenyekiti UWT Mkoa wa Kigoma alipokuwa akitoa salamu kwenye maadhimisho siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma Aggrey Magwaza Mkuu wa wilaya  ya Kibondo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma   Muhingo Mwemezi Kigoma Imeelezwa Wanawake wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kukosa elimu mapambano dhidi ya rusha za ngono hatua ambayo imekuwa ikididimiza ndoto za watu wengi hasa Wasichana na wanawake vitendo ambavyo vimekuwa vikishamili kila uchao Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Kibondo mwakilishi wa Mkuu wa Takukuru Mkoa huo Sweetberita Nkoba amesema yapo madhara ambayo yamekuwa yakiwakuta wanawake kutokana na Rushwa ya Ngono ambapo Taasisi yake imekuwa ikitoa elimu kwenye jamii ili iweze kuepukana na na vitendo hivyo na kusisitiza jamii kuacha...