Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2026

MANISPAA YA ILEMELA YAENDELEZA MPANGO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI KWA KUTOA TSH 625 KWA ROBO YA TATU 2026 10% MAKUNDI MAALUM

Picha
  Watu milioni 800 duniani wanatajwa kuishi katika umaskini uliokithiri na aina nyingi za umaskini zinasababishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wasio na ajira ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, ambayo yameliweka suala la kupambana na umaskini kama lengo kuu kuzishauri nchi zote kuutokomeza umaskini Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, siku ya kupambana na umaskini inaadhimishwa kwa kuzingatia wito uliotolewa miaka 25 iliyopita ya kutambua ujuzi na ujasiri wa familia zinazoishi katika umaskini duniani kote, umuhimu wa kuwafikia Watu maskini na kuwawezesha kiuchumi Tanzania ni moja ya nchi Duniani ambayo inaendelea Mikakati ya kupambana na umasikini   kwa   kuwawezesha Wananchi kiuchumi ,kutokana na hatua hiyo, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imeendeleza mpango huo ambapo katika robo ya tatu 2026 Vikundi 41 Vimepatiwa Mikopo ya 10%   amebainisha Kaimu Afisa Maendeleoa Manispaa hiyo Yusuph Okoko wakati wa hafla ya utoaji hudi ...

WATUMISHI SITA IDARA YA AFYA MKOANI KIGOMA WAMEKUFA MAJI ZIWA TANGANYIKA

Picha
  Watu sita ambao ni watumishi wa idara ya afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamethibtika kufa, watatu wakiwa bado hawajapatikana wengine tisa wakiokolewa wakiwa hai baada ya boti waliokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Kalalangabo wilayani humo. Akithibitisha vifo hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, amesema tukio hilo limetokea mapema leo Ijumaa Machi 13, 2026 asubuhi, wakati watumishi hao wakisafiri kwenda kijiji cha Kagunga kwa ajili ya kutoa chanjo kabla ya boti yao kupigwa na dhoruba kufuatia upepo mkali na kupinduka. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi Michael Maganga, amesema zoezi la kuwatafuta watu watatu watumishi wa idara ya afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, miongoni mwa waliopinduka na boti katika Ziwa Tanganyika eneo la Kalalangabo bado linaendelea. Aidha Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kigoma ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, imepiga ka...

Magu yapunguza vifo vitokanavyo na uzazi asilimia 70 kwa miaka mitano

Picha
  Mwanza . Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza imefanikiwa kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi   kutoka vifo 112 hadi 42 katika kipindi cha miaka mitano baada ya serikali kuboresha huduma kwa kutoa vifaa na kuongeza miundombinu ya majengo Voronica Gibson Mkazi wa Magu Hellen Chizere Muuguzi mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Magu Raphaem Mhana Mganga Mkuu W ya Magu Raphael Mhana Mganga Mkuu Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ameeleza kipindi cha2015hadi 2020,   hali ilikuwa hairidhishi ikilinganishwa na takwimu kuanzia 2020 hadi 2025   baada ya kufanyika   maboresho katika sekta ya Afya Hata hivyo Mhana amesema kutokana na maboresho hayo kwa sasa wanatengeza na Miguu bandia ambayo inasaidia Watu wanaopata matatizo mbalimbali zikiwemo ajali ‘’Wagonjwa wenye Matatizo ya Viungo hasa Miguu walemavu wa kuzaliwa na wanaokuwa wamepata ajali katika Wilaya ya Magu na maeneo ya jirani,wamekuwa wakisafiri kwenda mbali kutafuta huduma ya Miguu bandia lakini kwa hivi sasa   baada...