HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE
Muhingo Mwemezi Kibondo Baraza la Halmashauri ya Kibondo na Kikao cha ushauri cha Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma vimepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la Muhambwe kuwa majimbo mawili kwa kile kinachotajwa kuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi Daniel Ndalangavye ni Afisa uchaguzi halmashauri ya kibondo yeye katika taarifa yake anasema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa na Tume huru ya uchaguzi Tanzania ikiwa baadhi yake ni Idadi ya Watu, Ukubwa wa Eneona ukusanyaji wa ushuru na kodi huku akieleza kuwa kulingana na Jiografia ya eneo wananchi wengi wamekuwa wakipata usumbufu kuifikia ofisi ya Mbunge kwa sasa kutokana na umbali hivyo Jimbo likigawanywa Wabunge wa Majimbo hayo wataweza kuwahudumia wananchi kwa ufasaha zaidi Awali Jimbo la Muhambwe liliitwa Kibondo na mwaka 2010 likagwaanywa Majimbo mawili Buyungu Kakonko baadae kuitwa Muhambwe na sasa inapendekezwa Muhambwe kugawanywa tenda ambapo wajumbe wajumbe wa Baraza na Kika...

Maoni
Chapisha Maoni