HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

 

























 

Muhingo Mwemezi Kibondo

Baraza la Halmashauri ya Kibondo na Kikao cha ushauri cha Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma vimepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la Muhambwe kuwa majimbo mawili kwa kile kinachotajwa kuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi

Daniel Ndalangavye ni Afisa uchaguzi halmashauri ya kibondo yeye katika taarifa yake anasema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa na Tume huru ya uchaguzi Tanzania ikiwa baadhi yake ni Idadi ya Watu, Ukubwa wa Eneona ukusanyaji wa ushuru na kodi huku akieleza kuwa kulingana na Jiografia ya eneo  wananchi wengi wamekuwa wakipata usumbufu kuifikia ofisi ya Mbunge kwa sasa kutokana na umbali hivyo Jimbo likigawanywa  Wabunge wa Majimbo hayo wataweza kuwahudumia wananchi kwa ufasaha zaidi

Awali Jimbo la Muhambwe liliitwa Kibondo na mwaka 2010 likagwaanywa Majimbo mawili Buyungu Kakonko baadae kuitwa Muhambwe na sasa inapendekezwa Muhambwe kugawanywa tenda ambapo wajumbe wajumbe wa Baraza na Kikao cha ushauri wanapendekeza majina mapya yanayotakiwa kutumika baada ya Mgawanyo    Insert Paul Ngomagi

Katika Kikao cha Baraza la MadiwaniPaul Ngomagi alipendekeza liwepo Jimbo la Kibondo Mashariki na Kibondo Maghari huku baadae kwenye Kikao cha ushauri wilaya Mjumbe wa Kikao hicho Philbath Misuzi alipendekeza  Jimbo Jipya liitwe Muhambwe Magharibi na Jimbo la zamani liitwe Muhambwe Mashariki

Vikao vyote viwili kwa nyakati tofauti viliridhia kugawanywa kwa jimbo la Muhambwe huku Mkuu wa Wilaya ya Kibondo mwenyekiti wa Kikao cha ushauri Aggrey Magwaza akieleza kuwa mapendekezo hayo yanapelekwa kwenye vikao vya maamuzi kwa hatua zaidi hivyo taarifa zitatolewa baada ya maamuzi

Wilaya ya Kibondo ina jimbo moja la uchaguzi na Halmashauri moja  ambapo baadhi ya washiriki wa vikao hivyo Shedrack Chongera na Ladbod loki Katobahemu wakieleza kuwa  hatua hiyo iatasaidia kupunguza adha kubwa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii kwenye ofisi za umma

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu