Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2025

MIRADI YA MAJI THAMANI YA FEDHA IONEKANE

Picha
  Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko   Muhingo Mwemezi Kigoma Kutokana na serikali kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji Miundombinu   ya Maji, Wasimamizi wa Miradi hiyo wametakiwa kuahakikisha thamani ya fedha hizo inaonekana ili kuleta tija na kuondoa changamoto kwa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta Maji na kushindwa fanya shughuli za uzalishaji Kadri Miradi inavyoongezeka vivyo hivyo na migao ya Maji ipungue kwenye maeneo ya wananchi na huduma ziwe bora ikiwa ni pamoja na ankala halisi zinazotakiwa kulipwa na wananchi Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma Evance Malasa, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya Maji yaliyofanyika Kijiji cha Nyanzige kata ya Nyamtukuza ambapo amesema ni vema Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa wilayani humu kujitathimini na kufanya maboresho ya utoaji wa   huduma za Maji Maadhimisho hayo yameambatana na uwekaji jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi Mkubwa...

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Picha
    Muhingo Mwemezi Kibondo Baraza la Halmashauri ya Kibondo na Kikao cha ushauri cha Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma vimepitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo la Muhambwe kuwa majimbo mawili kwa kile kinachotajwa kuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi Daniel Ndalangavye ni Afisa uchaguzi halmashauri ya kibondo yeye katika taarifa yake anasema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa na Tume huru ya uchaguzi Tanzania ikiwa baadhi yake ni Idadi ya Watu, Ukubwa wa Eneona ukusanyaji wa ushuru na kodi huku akieleza kuwa kulingana na Jiografia ya eneo   wananchi wengi wamekuwa wakipata usumbufu kuifikia ofisi ya Mbunge kwa sasa kutokana na umbali hivyo Jimbo likigawanywa   Wabunge wa Majimbo hayo wataweza kuwahudumia wananchi kwa ufasaha zaidi Awali Jimbo la Muhambwe liliitwa Kibondo na mwaka 2010 likagwaanywa Majimbo mawili Buyungu Kakonko baadae kuitwa Muhambwe na sasa inapendekezwa Muhambwe kugawanywa tenda ambapo wajumbe wajumbe wa Baraza na Kika...

RUSHWA YANGONO BADO NICHANGAMOTO KWA WANAWAKE NA WASICHA KATIKA MASUALA YA MAENDELEO

Picha
Baadhi ya Wanawake walioshiriki maadhimisho siku ya Wanawake Duniani March8,2025 Hidaya Kimpwi Mkazi wa Buhigwe Aggripina Buyogela Mwenyekiti UWT Mkoa wa Kigoma alipokuwa akitoa salamu kwenye maadhimisho siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma Aggrey Magwaza Mkuu wa wilaya  ya Kibondo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma   Muhingo Mwemezi Kigoma Imeelezwa Wanawake wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kukosa elimu mapambano dhidi ya rusha za ngono hatua ambayo imekuwa ikididimiza ndoto za watu wengi hasa Wasichana na wanawake vitendo ambavyo vimekuwa vikishamili kila uchao Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Kibondo mwakilishi wa Mkuu wa Takukuru Mkoa huo Sweetberita Nkoba amesema yapo madhara ambayo yamekuwa yakiwakuta wanawake kutokana na Rushwa ya Ngono ambapo Taasisi yake imekuwa ikitoa elimu kwenye jamii ili iweze kuepukana na na vitendo hivyo na kusisitiza jamii kuacha...