RUSHWA YANGONO BADO NICHANGAMOTO KWA WANAWAKE NA WASICHA KATIKA MASUALA YA MAENDELEO
Baadhi ya Wanawake walioshiriki maadhimisho siku ya Wanawake Duniani March8,2025 |
![]() |
Hidaya Kimpwi Mkazi wa Buhigwe |
Aggripina Buyogela Mwenyekiti UWT Mkoa wa Kigoma alipokuwa akitoa salamu kwenye maadhimisho siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma |
Aggrey Magwaza Mkuu wa wilaya ya Kibondo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma |
Muhingo Mwemezi Kigoma
Imeelezwa
Wanawake wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kukosa elimu mapambano dhidi ya
rusha za ngono hatua ambayo imekuwa ikididimiza ndoto za watu wengi hasa
Wasichana na wanawake vitendo ambavyo vimekuwa vikishamili kila uchao
Akiongea
kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika
Wilaya ya Kibondo mwakilishi wa Mkuu wa Takukuru Mkoa huo Sweetberita Nkoba
amesema yapo madhara ambayo yamekuwa yakiwakuta wanawake kutokana na Rushwa ya
Ngono ambapo Taasisi yake imekuwa ikitoa elimu kwenye jamii ili iweze kuepukana
na na vitendo hivyo na kusisitiza jamii kuacha ukimya
Wakati wa
maadhimisho hayo baadhi ya Wazazi ambao ni Rebeca Mudala Mkazi wa Kibondo na
Hidaya Kimpwi Mkazi wa Buhigwe wamesema licha ya vitendo hivyo kufanyika kwa
siri sana wamesema wanaendelea kutoa elimu kwa watoto wao huku wakiomba vyombo
vinavyoa maamuzi kutenda haki pale watu wanapobainika kujihusisha na ukatili
‘’Kumekuwepo
na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakielekezwa kwenye mamlaka mbalimbali
kuanzia ngazi za vijiji kutotenda haki kwa kuwakingia vifua wakosaji huku
wahanga wa ukatili wakiendelea kutesema hivyo vitendo hivyo havikubaliki na ni
vema haki iwe inatendeka ili kujenga Imani kwa mamlaka za kutoa maamuzi’’ amesema
Hidaya
Hata hivyo
Mkoa wa Kigoma katika kutoa elimu ya Kisheria kupitia Kampen ya Sami Legal Aid
imeweza kutataua migogoro 920 ilipokelewa na kushugulikiwa 157 ilishughulikiwa
papo kwa papo na migogoro793 ilielekezwa katika mamlaka husika ili itatuliwe
hapa ameeleza Mkuu wa wilaya ya Kibondo Aggrey Magwaza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aliyekuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
Magwaza
ameongeza kuwa lengo la Kampeni hiyo ni kujenga uelewa kwa wananchi ili waweze
kujitambua na kuwa na matumizi mazuri ya masuala ya sheria na kutambua haki zao
hatua ambayo itasaidia kupunguza Migogoro isiyokuwa na sababu kwenye jamii
Maoni
Chapisha Maoni