MIRADI YA MAJI THAMANI YA FEDHA IONEKANE
Muhingo Mwemezi
Kigoma
Kutokana na serikali kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji Miundombinu ya Maji, Wasimamizi wa Miradi hiyo wametakiwa kuahakikisha thamani ya fedha hizo inaonekana ili kuleta tija na kuondoa changamoto kwa wananchi kutumia muda mwingi kutafuta Maji na kushindwa fanya shughuli za uzalishaji
Kadri Miradi inavyoongezeka vivyo hivyo na migao ya Maji ipungue kwenye maeneo ya wananchi na huduma ziwe bora ikiwa ni pamoja na ankala halisi zinazotakiwa kulipwa na wananchi
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma Evance Malasa, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya Maji yaliyofanyika Kijiji cha Nyanzige kata ya Nyamtukuza ambapo amesema ni vema Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa wilayani humu kujitathimini na kufanya maboresho ya utoaji wa huduma za Maji
Maadhimisho hayo yameambatana na uwekaji jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Maji ulioko kwenye kijii cha Nyanzige wenyethamani tsh 1.13 bilion ambao utasaidia kuhudumia wananchi 14 elfu wa Vijiji vine na hapa baadhi ya wananchi ambao ni Eleonora Josephat na Paul Kadumagiwapongeza kwa ujenzi wa mradi huo
Respichius Kahamba ni Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kakonko yeye amesisitiza utunzaji wa miundombinu na ulipaji wa Akala za Maji kwa wakati
Maoni
Chapisha Maoni