Ukubwa wa Mpaka wa Mkoa wa Kigoma chanzo Njia za Panya nyingi na kuingiza Wageni haramu
| Toyi Silvesta Diwani Kata ya Gwanumpu Kakonko Kigoma akiongea na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhala |
Ukubwa wa Mpaka wa Mkoa wa Kigoma chanzo Njia za Panya nyingi na kuingiza Wageni haramu
Kigoma;Kutokana na Mkoa wa Kigoma kuwa na Mpaka mrefu sana kuliko Mikoa yote ya
pembezoni huku vituo rasmi vya uhamiaji vikiwa mbali mkubwa toka kituo kimoja hadi kingine hatua inayodaiw a kupelekea uwepo wa njia za panya nyingi na wahamiaji haramu
kupata ulaisi wa kuingia nchini jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Tanzania
Mkoa huo unapakana na Nchi za
Burundi na Congo DRC upande wa Magharibi na nchi hizo zimekuwa zikikumbwa na
matatizo ya usalama na kupelekea Raia wa nchi hizo
kukimbia kutafuta sehemu salama
Raia wa Nchi jirani wanadaia kuingia Tanzania kwa Vigezo vya kutafuta
vibarua kupata Mkate katika maeneo vya Vijiji vya Mpakani Mkoani Kigoma na
baadae ulazimika kuendelea kukaa Vijijini humo kinyume cha sheria za
Tanzania na wengine uingia nchini
kufanyabiashara katika Masoko ya ujirani mwema yaliyoko Mipakani kasha kuingia
Vijijini
Wenyeji hudaiwa kuwapangisha katika Nyumba za Makazi na baadae kununua
ardhi na kuishi kama wenyeji kinyume na taratibu huku vitendo visivyofaa
vikiendelea kutendeka
Kutokana na hali hiyo Kata ya Gwanumpu iliyoko Wilayani Kako Mkoani
Kigoma imeanza udhibiti wa wahamiaji haramu kuendelea kuingia nchini na kuishi kinyume cha sheria ambapo Viongozi
wenyewe kuanzia ngazi za Vijiji wameanza kudhibitiana ambapo katika Kikao cha
Viongozi wa Kata hiyo Kikiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Toy Silvesta,,Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo Rashid Ahnmed amewaeleza Viongozi kuanzia ngazi za
Vitongoji wanaowapangisha wahamiaji kuwaondoa mara moja kabla hatua hazijaanza
kuchukuliwa
‘’Hatuwezi kuanza kuwaandama wananchi wakati wapo Viongozi wanaosadikiwa
kuwahifadhi wahamiaji haramu na hicho ndicho chanzo cha kuanza upotevu wa amani’’
amesema Shadi
Akiwa kwenye Mkutano wa hadhala akiongea na Wananchi Diwani wa Kata hiyo
Toyi Silvesta amewashauri wananchi kuacha Tabia ya kuwakumbatia wahamiaji
haramu maana ni kinyume na sheria za Nchi na atakaekutwa anawaifadhi watu hao
atachukuliwa hatua na Masoko yote ya Mpakani lazima mwisho iwe saa kumi na
mbili jion
Toyi ameongeza kuwa kumekuwepo na tabia ya kuoleana kiholaholela hatua
inayochangia kuongezeka wageni hao huku wengine wakiingia naa Mifugo na
kusababisha magomvi kati yao na wageni hao
Baadhi ya Wananchi wameeleza kuwa ni vema serikali kupitia Idara ya
uhamiaji ingeweka Doria za Mara kwa
mara kwenye Vijiji ili kudhibiti hali
hiyo kwani wapo wageni hao ambao wamekuwakijificha vijijini na wengine
walishapewa uongozi kwenye serikali za Vijiji na kwenye vyama vya siasa
Maoni
Chapisha Maoni