DC MISUNGWI AHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUANDIKISHA WATOTO MASHULENI KWA WAKATI
DC MISUNGWI AHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUANDIKISHA WATOTO MASHULENI KWA WAKATI
![]() |
| Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi |
![]() |
| Mary Mussa Mwalimu Shule ya Msingi Misungwi |
![]() |
| Klaud Richard Mkazi wa Misungwi |
ya Misungwi Mkoani Mwanza kuendelea kufanya vizuri katika uandikishaji wa Wanafunzi Elimu awali na Msingi, bado hamasa inahitajika kutolewa kufia malengo yanayokusudiwa
Matarajio ya mwaka 2026 kwa Elimu awalini ilikuwa ni kuandikisha Watoto 13219 na walioandikishwa hadi sasa ni 6403 huku dara la Kwanza wanatarajia kuandikisha Wanafunzi 14551 na mpaka sasa Watoto 9082 wamekwisha
kuandikishwa wakati zoezi likiendelea
Akiongea Ofisini na Waandishi wa Habari Kwake Mkuu wa Wilaya Misungwi Johari Samizi ameeeleza uandikishaji wanafunzi unavyoendelea na
maelekezo yote yametolewa kwa Viongozi wa Vitongoji Vijiji na Kata,
kuwaelimisha Wananchi na mchakato huo unaendelea vizuri
Samizi ameendelea kuwahamasisha Wazazi na Walezi kupeleka watoto wao
waandikishwe kwa wakati kabla shule hazijafunguliwa ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha wanafunzi 7019
waliochaguliwa kunza kidato cha kwanza mwaka 2026,wanaripoti kwa wakati
‘’Kama inayohamika Wakazi wa eneo letu hili wanajishugulisha na ufugaji
na Kilimo hatua ambayo upelekea baadhi ya Wazazi kuwatumia Watoto wanaotakiwa
kuwa mashuleni kufanya shughuli hivyo
nawahimiza kila mmoja kuhakikisha Mtoyo
wake anapata Elimu’’ ameeleza Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi
Klaud Richard na Bakari Husein ni baadhi ya Wazazi na walezi Wakazi wa
Misungwi wameeleza kuwa wamejipana kuhakikisha
watoto wanapata elimu kwani ni wjibu wao kama wazazi huku mmoja wa walimu wa shule ya Msingi
Misungwi Maria Mussa akieleza katika shule yake zoezi la uandikishaji
linaendelea vizuri japo shule bado hazijafunguliwa



Maoni
Chapisha Maoni