Walemavu katika Wilaya ya Kibondo mkoani kigoma wamelalalmikia tabia ya baadhya ya wakuu wa shule za MSINGI na sekondari ya kutowapokea watoto walio na ulemavu kwa viungo vya mwili kwa madai ya kutokuwepo kwa walimu walio na uwezo wa kufundisha watoto walio na hali hiyo.




Walemavu katika Wilaya ya Kibondo mkoani kigoma wamelalalmikia tabia ya baadhya ya wakuu wa shule za MSINGI na sekondari ya kutowapokea watoto walio na ulemavu kwa viungo vya mwili kwa madai ya kutokuwepo kwa walimu walio na uwezo wa kufundisha watoto walio na hali hiyo.

Hayo yaliwekwa  wazi jana na Joseph Slivester  mmoja wazazi wakatiwa watoto wenye ulemavu wakati wa kikao cha semina elekezi kwa wazazi na walezi wa   watoto wenye ulemavu semina iliyoandaliwana shirika linalojishughulisha na wanawake pamoja na watoto wa kike wenye ulemavu liitwalo tekra lenye makao yake makuu mjini bukoba Mkoani Kagera.kwa lengo la kuwaelimisha wazazi wa watoto wenye ulemavu umuhimu wa kusomesha waelemabu

Alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wakuu wa shule kutowapokea watoto hao kwa madai ya kutokuwepo kwa walimu walio na uwezo waufundisha watoto walio na ulemavu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu inayoendana hali waliyonayo  hatua ambayo wamesema inapelekea watoto hao kukosa haki zao kushinda nyumbani bila kusoma kutokana na kurudishwa Majumbani.


Kwa upande wake analice Lubago ambae ni mlemavu wa macho pamoja na Bw, Nashon Amos mwalimu elimu maalum walishauri ni vema wazazi wakawapeleka watoto wao shule licha ya kutokuwepo kwa miundimbinu rafiki pamoja na walimu hao kutowapokea watoto hao ili waweze kupatiwa elimu ambayo itawasaidia hapo baadae hasa kwa kuwasiliana na maafisa Elimu na vingozi katika maeneo yao kama waratibu elimu na watendaji kwa maelekezo zaidi
.
Mratibu wa shirika la Tekra kutoka mjini Bukoba Bw. Kasaju mugisha amesema kuna faida za mtoto mwenye ulemavu kuchanganyika na watoto wasiokuww na ulemavu ikiwa ni pamoja na kuondoa dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuwa watu walio na ulemavu wamesahaulika katika jamii.


Hata  hivyo mwenyekiti wa chama cha walemavu wilaya ya kibondo Evalist Ngaramaamesema kuwa licha ya kudaiwa kuwepo kwa vikwazo hivyo, wapo baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwaficha watoto walemavu hatua ambayo imekuwa ikikwamisha juhudi za kuwatambua ili wapate huduma huku afisa elimu maalum wilaya kibondo Bw Gabliel Ntambala, akielekeza kuwa mtoto akifikishwa shule yoyote ataelekezwa pa kumpeleka kulingana na tatizo alilonalo


Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Kibondo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo bw.Charles Mwanasawe amesema endapo mwalimu yeyote atabainika kuhusika na tuhuma hizo atachukuliwa hatua za kisheria ambapo amewataka wazazi hao kutoa taarifa kwa viongozi pale wanapo baini kufanyiwa vitendo hivyo.


Wilaya ya kibondo  inakadiliwa kuwa na idadi ya watoto  walemavu wapatao 200 lakini waliokwisha tambulika ni 60 tu hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na jamii kuwa wazazi ndio chanzo kikubwa kwa kuwaficha na kuwakosesha haki na shule zilizoainishwa kuwapokea watoto wa mahitaji maalum ziko tano ikiwa Kifura,Mabamba,Kibondo Kumwabu na Migezi

Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao