Mila Potofu sababu uharibifu wa Mazingira Kibondo

 






Kibondo. Uchomaji Moto Mistu ni moja ya sababu zinazopelekea uharibifu wa Mazingira kwa Kiwango kikubwa licha ya jitiada nyingi zinazofanyika kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma

Indaiwa kuwa, Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wanalazimika kutumia Imani inayoshangaza kuchoma Moto sehemu yoyote  kwa kujipima urefu wa maisha yao ambapo Mtu akiwasha Moto ukasambaa eneo kubwa ndiyo naye ataishi maisha marefu

Stephan Janks ambaye ni Afisa Mazingira Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma akiwa katika uzinduzi wa Kampeni ya upandaji Miti iliyofanyika Kiwilaya jana  kwenye Kijiji cha Kumhama Kata ya Bitare amesema kwa Mwaka jana kati ya Miti 90,000 iliyopandwa katika maeneo mbalimbali Miti 50 ,000 ilichomwa Moto na kuharibiwa kabisa na mingine kung’olewa lewa kabisa na kuchukuliwa na wananchi

Janks aliongeza uwa wamekuwa wakifanya jitiada kubwa kuhakikisha wananchi wengi wanapanda Miti lakini baadae uharibiwa na baadhi ya ikiwa ni pamoja na king’oa na kwenda kuipanda sehemu nyingine bila utaratibu na kuchunga mifugo kwenye maeneo ilikopandwa Miti hiyo

Mmoja wa Wadau wa uhifadhi wa Mazingira ambalo ni Shirika la Danish Refugee Council  linalotoa huduma kwa wakimbizi Mkoani ambalo liliwakilishwa na Meneja wake Alfred  Magehema amesema wanatarajia kupanda miti million moja na laki sita kwa mwaka 2022  katika wilaya za Kakonko Kasulu na Kibondo huku wakati wa uzinduzi wa kampeni ikipandwa miti 65,000 katika hekali 100

‘’Kibondo tunatarajia kupanda Miti laki nane na hasini, Wilaya ya Kakonko Miti 320,000 na Kasulu tutapanda Miti 430,000 ambapo mwaka jana 2022 tulipanda Miti 560,000 kwa Wilaya zote tatu ikiwa lengo ni kuunga Mkono jitiada za serikali katika utunzaji wa Mazingira’’alisema Magehema

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza,aliyekuwa mgeni rasmi na kuongoza zoezi hilo, amewataka Wananchi kulindana Mazingira kwa kuwataja wanaochoma Moto Mistu yakiwemo Mazao ya Watu Mashambani ili hatua zichukuliwe

Kuendekeza Mila Potofu ni moja ya sababu zinazopelekea uwepo wa uchomaji Moto hali ambayo imekuwa ikisababisha hasara kubwa watu wengine wasiyokuwa na hatia ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Agrey Magwaza,aliwataka Wananchi kuchana na tabia hizo kwani hakuna anayeweza kupima urefu wa maisha Mtu kwa njia za namna yoyote ile bali mwenye uwezo huo ni Mwenyezi Mungu peke yake

Hata hivyo baadhi ya Wananchi walioshiriki kwenye uzinduzi huo, ambao ni Omary Hamis na Ruth Epafra, walisema hali hiyo inasababishwa na uzembe wa baadhi ya Viongozi kushindwa kusimamia sheria zilizopo kwani Watu wanaochoma Moto  Mistu,wengi huwa wanafahamika lakini hatua hazichukuliwi

‘’licha ya elimu kutolewa lazima usimamizi mzuri wa shria uwepo kwani kumekuwepo watu wanaofanya uharibifu lakini hawachukuwi hatua licha ya kufahamika, hivyo hali hiyo ikiachwa iendelee basi hakuna sababu ya kuendelea kuhamasisha  watu kupanda miti tena kwa garama kubwa na baada ya muda mfupi inaharibiwa wakati uwezekano wa kuzuia hali hiyo ulikuwepo’’ alisema Omary

Mwicho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji