KAMATI YAITAKA TANROADS KUZINGATIA VIPENGELE VYA GHARAMA KWENYE MIRADI
KAMATI YAITAKA TANROADS KUZINGATIA VIPENGELE VYA GHARAMA KWENYE MIRADI Na Mwandishi Wetu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuhakikisha wanaingia mikataba ya ujenzi yenye gharama isiyokuwa na nyongeza za fedha. Imesema wakandarasi wengi wanaoingia mikataba ya ujenzi na Tanroads wanakuja na mfumo wa nyongeza za gharama hali inayoisababishia serikali gharama zisizokuwa na tija. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seleman Kakoso alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya mradi wa Dart awamu ya pili eneo la Mbagala. "Serikali imetoa fedha nyingi katika ujenzi wa mradi huu. Jitihada ni nzuri zimefanyika, tumeridhika na kwa sasa kuna maendeleo. Lakini igeni mfumo wa TRC katika ujenzi wa barabara. Wakandarasi wanakuja na mfumo wa nyongeza za gharama hali inayosababisha miradi kuwa na gharama kubwa," alisema Kakoso. Mbali na kutoa agizo hilo, kamati hiyo iliagiza Ta...