MTABILA YAONGEZA UZALISHAJI
Kasulu. Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mtabila kilichopo Wilayani Kasulu mkoani Kigoma, kimefanikiwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo bustani na ufugaji, na kuwezesha vijana wanaopata mafunzo ya Kijeshi kikosini hapo, kuwa na uwezo wa kujitegemea kutafuta fursa za kujiajili kupitia kilimo.
Katika mahafari ya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Oparesheni Jenerali Venance Mabeyo, Ambapo baadhi ya vijana Julias Masuna Jesca Jeremia jana wamesema stadi za maisha wanazofundishwa kikosini humo, zimewawezesha kuongeza uzalishaji wa mazao.
''Nilifika hapa Kikosini 825 nikiwa sifahamu mambo mengi yahusuyo maisha hasa katika masuala ya maendeleo na kujituma hasa katika sekta ya kilimo ila nilipokutana na wataalam wa Kilimo nimeweza kujifunza namna ya kuendesha kilimo kwa njia za kisasa hata matumizi ya mbolea hatua ambayo naamini itanisaidia baadae katika shuguli zangu hivyo naishukuru serikali kwa kunipatia fursa hii''alisema Julias mhitimu
Afisa Kilimo katia Kikosi hicho Philmon Mkude aliongeza kuwa takribani miaka miwili iliyopita uzalishaji wa zao la mahindi ulikuwa chini ambapo kwa msimu mmoja walikuwa wanaweza kuzalisha magunia 400 ila katika msimu uliopita wameweza kuzalisha Gunia 1000 na uzalishaji huo umekuwa ukiendeshwa na Vijana wanaopata mafunzo Kikosini hapo
Kwa upande wake Kamanda Kikosi 825 KJ Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya amepongeza umahili wa vijana katika kufanya kazi za uzalishaji mali kikosini, wakati mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Izack Mwakisu aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka vijana hao, kuwa wazalendo wa kulitumikia Taifa kutokana na mafunzo waliyoyapata.
Mkuu wa mafunzo Jeshi la Wananchi Brigedia Jenerali Charles Ndiege aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi, amewataka wahitimu wa mafunzo ya Jeshi kuwa na bidii kwa kulitumikia Taifa katika shughuli za uzalishaji, Wakati Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Aisha Matanza akiwataka kuwa mabarozi wa kusaidia jamii na Taifa.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni