WALIMU ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAOEA ILI KUBORESHA ELIMU
WALIMU ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAOEA ILI KUBORESHA ELIMU
Kibondo.Katika
kurekebisha upatikanaji wa elimu hapa nchini walimu wamehaswa kuacha tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea ili kufikia
malengo ya serikali na kuwapatia Watoto ujuzi
Hayo
ameyasema na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi upande wa Elimu Charles
Msonde alipokuwa akizungumza na Walimu wa shule za Msingi na sekondari wilayani
Kibondo Mkoani Kigoma ambapo amesema Mkoa huo uko kiwango cha chini kielimu
kutokana na ufundishaji usiozingatia vigezo
Amesema kila
mwalimua anatakiwa kujipima utendaji wake wa kazi kwa kuwasaidia wanafunzi na
kuwataka kuacha mazoea kazini
Aidha Msonde
ameeleza kusikitishwa kwake juu ya halimu ya elimu ilivyo wanafunzi shule za
Msingi wanapanda Madarasa wakiwa hawajui kusoma wala kuandika huku walimu
katika shule zinazomilikiwa na serikali wakiona ni mambo ya kaiwada na kuwahasa
kuchukua hatua
‘’Wanafunzi
katka shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi channe wengi wao
wamekuwa wakikwama katika masomo yao kutokana na kushindwa kuelewa lugha ya
kujifua ambayo ni Kiigereza ambapo wengi hushindwa kujieleza huku walimu
wakikimbizana na kumaliza Mada tu ambazo wanafunzi hawazielewi hivyo nawaomba
walimu kuweni makini katika kuboresha elimu’’alisema Msonde
Baadhi ya
walimu walioshiriki kikao hicho Jose Paschal anaefundisha shule ya Msingi
Kibondo na John Kimasa shule ya Msingi Boma wamekili uwepo wa utendaji
usioridhisha na baada ya kupata maelekezo wameahidi kufanya kazi kwa bidii na
maarifa
Pamoja na
mambo mengine Msonde ameitaka halmashauri ya kibondo kutatua mahitaji ya walimu
na kuacha kutumia lugha zisizo rafiki walimu wanapopeleka changamoto zao ili zitatuliwe ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
wanamaliza malalamiko yote ya Walimu ili wasikate tamaa
Charles M sonde Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Upande wa Elimu alipokuwa akizungumza na Walimu wa shule za Msingi na Sekondari kwenye Ukumbi wa Kibondo shule ya sekondari ya Wasichana |
Baadhi ya Walimu walishiriki Kikao na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Charles Msonde |
Maoni
Chapisha Maoni