Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2024

KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO

Picha
  KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi, Godfrey Kasekenya amewataka vijana Wilayani Ileje, mkoani Songwe kujikita kwenye michezo na kutumia fursa ya mashindano ya kombe la Kasekenya kuimarisha afya, ushirikiano na kukuza vipaji. Akizindua Bonanza la kuhamasisha michezo Wilayani huko, Mbunge Kasekenya amesema wilaya hiyo imedhamiria kuwekeza kwenye michezo ili kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kupata ajira. "Mashindano haya yatumike kama chachu ya kuhamasishana kufanya kazi kwa bidii na kukuza vipaji kwani michezo ni ajira, afya na urafiki", amesema Mhandisi, Kasekenya. Aidha, Kasekenya amesema kuwa Mashindano hayo pamoja na mambo mengine yanahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura, kugombea na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu. Amefafanua kuwa Bonanza hilo ambalo ni uzinduzi wa Kasekenya Cup limekutanisha timu za mpira wa miguu wanaume na wanawake, vikundi v...