KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO
KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi, Godfrey Kasekenya
amewataka vijana Wilayani Ileje, mkoani Songwe kujikita kwenye michezo
na kutumia fursa ya mashindano ya kombe la Kasekenya kuimarisha afya,
ushirikiano na kukuza vipaji.
Akizindua Bonanza la kuhamasisha michezo Wilayani huko, Mbunge
Kasekenya amesema wilaya hiyo imedhamiria kuwekeza kwenye michezo
ili kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kupata ajira.
"Mashindano haya yatumike kama chachu ya kuhamasishana kufanya kazi
kwa bidii na kukuza vipaji kwani michezo ni ajira, afya na urafiki", amesema
Mhandisi, Kasekenya.
Aidha, Kasekenya amesema kuwa Mashindano hayo pamoja na mambo
mengine yanahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura, kugombea
na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Amefafanua kuwa Bonanza hilo ambalo ni uzinduzi wa Kasekenya Cup
limekutanisha timu za mpira wa miguu wanaume na wanawake, vikundi
vya muziki wa asili, riadha, na uchezaji wa muziki ambapo washindi
wamejizolea zawadi mbalimbali.
Katika soka, timu ya Makaburu ya jimbo la Busokelo, mkoani Mbeya
imeifunga kombaini ya Sange iliyopo wilayani Ileje, mkoani Songwe bao 3
kwa 2 wakati wanawake Lubanda wakishinda kwa penati 3 kwa 2 dhidi ya
Kalembo FC baada ya sare ya bao 2 kwa 2.
Viongozi mbalimbali wa Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa wa Songwe wa
vyama na Serikali wameshiriki Bonanza hilo.
Maoni
Chapisha Maoni