Samia atoa msaada kwa Watoto wenye mahitaji maalum
Hapa Dc Malasa akikabidhi zawadi hizo kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum |
Baadhi ya Zawadi zilizotolewa |
Jesca Andason akitoa shukrania kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassani |
Ibrahimu Masumbuko Mwl Mkuu shule ya Msingi Nengo Elimu Jumuishi |
Samia atoa msaada kwa Watoto wenye mahitaji maalum
Muhingo Mwemezi Kibondo
Watoto
wenye Mahitaji maalum wanaoishi kwenye Nyumba maalum za kuwahifadhi watoto hao,
wanahitaji faraja kutoka kwenye jamii kwani nao wanauhitaji haki kama Binadamu
wengineambapo jamii imetakiwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali kusaidia
makundi hayo hapa nchini
Suala
la ulinzi wa Watoto hao linaihusu jamii yote kwani unyanyasaji dhidi yao,
unaanzia ngazi ya familia hivyo kila mmoja anatakiwa kutoa taarifa za uwepo wa
watu wenye viashilia vya unyanyasaji ili wadhibitiwe kabla ya kutimiza adhima
zao
Kanali
Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya ya Kakonko ambayeni Kaimu Mkuuu wa Wilaya ya
Kibondo Mkoani Kigoma amesema hayo wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali
kikiwemo chakula kwa Wanafunzi wenye Mahitaji maalu katika shule ya Msingi
Nengo ambapo ameeleza kuwa Watu wasiyokuwa na mapenzi mema na wanaotaka
kuwatendea ukatili Watoto hao mambo yao yanaanzia kwenye familia
Aidha
Malasa amesistiza jamii kuacha kuwaficha Watoto wenye ulemavu majumbani bali
wawaweke wazi ili serikali iweze kusaidia pale inapobidi hasa kuwapatia haki ya
elimu kwani nao wanaweza kulingana na hali Mtu ilivyo
Msaada
huowenye thamani ya sh 1,900,000/ umetolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya huku Mkuu
huyo wa Wilaya akitoa wito kwa walimu kuwajenga kimaadili watoto hao ili
kuondoa mitazamo hasi kwenye jamii dhidi yao
Nao
baadhi ya wanafunzi hao wenye mahitaji maalum wakatoa shukrani zao
wakiwakilishwa na Jesca Andason, huku Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Masumbuko
akitoa ombi kwa serikali kusaidia wanafunzi walemavu wa viungo kuwajengea njia
maalum kwani upata changamoto wanapotoka mabwenini kwenda Madarasani
Maoni
Chapisha Maoni