KUHITIMISHA UCHUKUAJI FOMU KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE JIMBOLA MUHAMBWE CCM

 

rAPHAEL SUMAYE KATIBU CCM WILAYA YA KIBONDO









Chama cha Mapinduzi Ccm kimehimisha zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania fafasi za Ubunge na Udiwani kamalilivyoanza June 28,2025 hadi leo julai 2,2025 kwa Wanachama wake kwa ajili ya uchaguzi Mkuu  kuwapata Madiwani,Wabunge na Rais unaotarajiwakufanyika octoba mwaka huu

 

Katika Jimbo la Muhambwe Kibondo Mkoani Kigoma,wamejitokeza Wananchama wa Ccm walioonyesha Nia ya kugombea ubunge  kuitia ccm idadi imetajwa ni 17  na wote wamerejesha fomu zao kwa wakati

 

 Aidha Sumaye amesema baada ya hatua hiyoya awali  itaendelea michakato mingine ili kifikia malengo yanayokusudiwa huku Waliochukua fomu kugombea udiwani Kata zote  ikitajwa idadi ni   wanachama 96 na hakuna malalamiko yaliyojitokeza  kwa madai ya kutotendewa haki

 

Jimbo la Muhambwe linaundwa na  Vitongoji  420,Vijiji 50 na Kata 19 huku baadhi ya watia ambao ni Adrian Thoma Andason Njiginya na Japhet Jakson wakieleza kuridhishwa na zoezi lilivyoendeshwa kwa amani na utulivu  bilaMizengwe yoyote

 

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HALMASHAURI YA KIBONDO KULIGAWA JIMBO LA MUHAMBWE

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

40 CHADEMA KIBONDO WAJIONDOA