Mnyukano Ubunge Muhambwe
![]() |
Jamal Abdlah Mwenyekiti Ccm Mkoa wa Kigoma achukua Fomu kugombea Ubunge Jimbo la Muhambwe |
![]() |
Frolence Samizi Mbunge Muhambwe anaetetea Kiti chake achukua fomu ubunge Muhambwe |
Kuelekea uchaguzi Mkuu
2025,Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
Ccm Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wameendelea kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani na
Ubunge kwa ajili ya uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu
Baadhi
ya wanachama hao mmoja wapo ni Mwenyekitiwa Ccm Mkoa wa Kigoma Jamali Abdalah
ambaye ametia nia ya kugombea nafasi ya
Ubunge katika Jimbo la Muhambwe Kibondo kwa kuchukua Fomu kwenye ofisi za Ccm
wilayani Kibondo
Frolence
Samizi ambaye ni Mbunge anaeteteaKiti chake nae amechukua fom kugombea nafasi
hiyo kwa mara nyingine tena huku wakifuatiwa na wanachama wengine Nduhilabusa
Mapigano Katibu Jumhiya ya Wazazi Wilaya ya Kasulu, Geradina Kabululu na wengine
Kwaupande
wake Katibu wa Ccm Wilaya ya Kibondo Rafael Sumaye amesema hadi kufikia mchana
wa leo Jen 30,2025, waliokuwa wamechukua
fom idadi yao ni kumi na moja huku akiwahamasisha wanachama wengine wenye sifa
kuwania nafasi za huongozi katika uchaguzi Mkuu
2025
Aidha
Sumaye ameeleza kuwa bado ofisi yake inaendelea kuwapokea watia Nia mpaka pale
muda uliopangwa kuhitimisha zoezi hilo hapo julai 2,2025
Maoni
Chapisha Maoni