Wanavijiji kata ya Mulungu wilaya ya kibondo uenda wakahitaji msahada wa chakula
Wanavijiji kata ya Mulungu uenda wakahitaji msahada chakula Wakazi wa vijiji vya Kumbanga na Kumuhasha, Kata ya Mulungu Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma uenda wakakumbwa na Baa la njaa mwaka huu baada ya jua kali na kukosa mvua za kutosha katika msimu wa kilimo mwaka jana hali iliyosababisha mazao kuharibika mashambani Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao ambao ni Astelia Adriano na Julias Paulo wote wakazi kumbanga mkazi wa Kumbanga kwa nyakati tofauti kutoka katika vijiji hivyo wakazi wa vijiji hivyo, wamesema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka jana hawakupata mvua za kutosha na kuwafanya wakulima kupata mavuno kidogo ya chakula ambapo wengi wao wanahofia kutofika kwenye msimu ujao wa kilimo wakiwa na chakula katika familia zao, tofauti na vipindi vilivyopita maana wamekuwa wakipata Gunia kati ya 40 hadi 50 kwa hekali moja ila msimu huu wengi wao wamepata gunia moja hadi 2 kwa hekali moja Wamedai kuwa hali hiyo imewahathi...