Lipumba ziarani Kigoma
Professor Ibrahim Lipumba mwenyekiti Cuf Taifa alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kibondo mkoani Kigoma katika mkutano wa hadhala |
Lipumba ziarani Kigoma
Kwakuwa mwaka huu wa 2015 ni mwaka wa uchaguzi katika nchi
ya Tanzania Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanajiandikisha kwa wingi katika
maene ambayo bado zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili
waweze kutimiza wajibu wao katika uchaguzi unaotarajia kufanyika October mwaka
huu
Hayo aliyabainisha Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Profeser Ibrahim Lipumba alipokuwa akiongea na Wananchi kwenye mkutano
wa hadala uliofanyika jana katika Viwanja vya Community mjini Kibondo
Lipumba alisema kuwa watanzania wanatakiwa kucha ushabiki
usiyokuwa na tija bali wanatakiwa kufanya uamzi wa mabadiliko kwa kuchagua
viongozi bora na wenye maadili na wale
watakao weza kulitumikia Taifa hili kwa moyo wa dhati kwani linakabiliwa na
changamoto nyingi
Aidha alisema kuwa Tanzania inatajwa kuwa na Raslimali
nyingi zinazoweza kuinfanya kuwa Tajiri lakini wananchi wake ni masini kuliko
inavyotakiwa kuwa kwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali za ukosefu wa Elimu
bora Afya , Maji safi na mambo mahitaji
mengi ya msingi huku akieleza kuwa hali hiyo inaweza kuatuliwa na viongozi
waadilifu na wenye uchungu na maenedeleo ya nchi hii
Pamoja na hatua
nyingine licha ya chadema kusimamisha
mgombea wa ubunge katika jimbo la muhambwe mwenyekiti wa chama cha Cuf taifa
professor Ibrahim Lipumba amesisitiza kuwa jimbo lenye mbunge ambaye chama
chake kimejiunga na ukawa ataendelea kupeperusha bendelea ya chama husika na
vyama vingine vitapaswa kumuunga mkono
Professor Lipumba amebainisha hayo wakati akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya community center kibondo
mjini Mkoani Kigoma jana na kwamba vyama vinne vinavyounda ukawa tayari
vimekubaliana kuachiana majimbo hivyo hakuna sababu yoyote kuona jimbo lenye
mbunge wa ukawa wakijitokeza wagombea wengine kutaka kuvuruga makubaliano
Aidha Professor Lipumba amesema kuwa katika majimbo ambayo
yako wazi wagombea kutoka vyama vya ukawa watachukua fomu na kuomba kuteuliwa
na atakayepata kura nyingi kati yao atapata nafasi ya kugombea na kuviwakilisha
vyama vingine ambapo itabidi aungwe mkono na vyama vilivyosalia
Pamoja na jimbo la muhambwe kuongozwa na mbunge kutoka chama
cha NCCR Mageuzi chama ambacho kimo katika umoja wa katiba ya wananchi lakini
hivi majuzi chama cha demokrasia na maendeleo chadema kilisimamisha mgombea wa
ubunge kinyume na makubaliano yao
Maoni
Chapisha Maoni