Jengo la Halmashauri ya wilaya Kibondo mkoani Kigoma liliungua na kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara kubwa ikiwa ni majengo na vitu mbalimbali
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni walinzi wa ofisi hizo waliokuwa zamu, ambao ni Musa Moshi Ndayimisi Gwakila wamesema kuwa muda wa saa saba usiku wa kuamkia leo waliona moto mkubwa ulio lipka kwa gafla katika jingo la masijala na wao kuchukua harua za kulitaalifu jeshi la Polisi kwa msahada zaidi
Judathadiusi mboya mkurugenzi mtendaji Halmashauri hiyo amekiri kuwepo kwa ajali hiyo, na kusema kuwa ofisi zilizoungua ni Utumishi, Masjala ya wazi naya siri pamoja na ofisi ya mkurugenzi na kuongeza kuwa vitu vyote vilivyokuwa katika ofisi hizo vimeteketea ikiwa nyaraka mbalimbali Samani za ndani na compute na kuongeza kuwa kuwa hasara haijafahamika niasi gani hadi pale atakapopatikana mtaalam ili kufanya tahmini
Ester Jackson na Ayubu Bagite, ni baadhi ya Wakazi wa mji wa kibondo waliofika katika eneo la tukio kudai kuwa moto huo uenda ungewza kuzimwa na kunusuru mali za umma lakini ilishindikana japo wengi walijitaidi kuzima hivyo kuiomba serikali kuleta kikosi cha zima moto katika wilaya hii ili kuepuka majanga kama hayo yanayoweza kujitokeza tena
Marko Joshua Ocd kibondo ameeleza namna alivyopata taarifa na kushugulikia tatizo hilo la kuzima moto japo ilishindika na kudai kuwa uchunguzi unafanyika ili kujua chanzo cha moto huo kama ni hitlafu ya umeme aula ili taratibu zifuatwe
Wilaya hiyo hadi sasawilaya kibondo haina Kikosi cha zimamoto pamoja na mabadiriko ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na ukuaji wa kiuchumi unaweza kusababisha mambo mbalimbali ikiwa ni majanga ya tofauti na zamani ikilinganishwa na sasa kuwepo kwa nishati umeme hku wakazi wengi wakiwa hawana elimu ya uzimaji moto na matumizi ya umeme majumbani
Mwisho
|
Mabaki ya ofisi za Halmashauri ya W Kibondo iliteketea Kwa Moto |
|
Ndayimisi Gwakila Mlinzi Shuhuda |
|
M. Joshua Ocd Kibondo |
|
J Mboya Ded Kibondo |
|
Ester Jakson Mkazi wa Kibondo |
Maoni
Chapisha Maoni