Wanavijiji kata ya Mulungu wilaya ya kibondo uenda wakahitaji msahada wa chakula
Wanavijiji kata ya Mulungu uenda wakahitaji msahada chakula
Wakazi wa
vijiji vya Kumbanga na Kumuhasha, Kata ya Mulungu Wilaya ya Kibondo mkoani
Kigoma uenda wakakumbwa na Baa la njaa mwaka huu baada ya jua kali na kukosa
mvua za kutosha katika msimu wa kilimo mwaka jana hali iliyosababisha mazao
kuharibika mashambani
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao ambao ni Astelia Adriano na Julias
Paulo wote wakazi kumbanga mkazi wa Kumbanga
kwa nyakati tofauti kutoka katika vijiji hivyo wakazi wa vijiji hivyo,
wamesema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka jana hawakupata mvua za kutosha na kuwafanya wakulima kupata mavuno kidogo ya chakula ambapo wengi
wao wanahofia kutofika kwenye msimu ujao
wa kilimo wakiwa na chakula katika familia zao,
tofauti na vipindi vilivyopita maana wamekuwa wakipata Gunia kati ya 40
hadi 50 kwa hekali moja ila msimu huu wengi wao wamepata gunia moja hadi 2 kwa
hekali moja
Wamedai kuwa
hali hiyo imewahathili hasa wazazi wenye wanafunzi kwani walikuwa wakitegemea
mazao hususa Mahindi na Maharage kwa ajili ya biashara ili
kulipia ada mashuleni.
Hata hivyo
Bi, Keldonia Kayella mkazi wa kijiji cha Kuuhasha alifafanua
kuwa kwa watu waliokosa kabisa mazao ya chakula kwa kutokupata mahindi na
Maharage hivi sasa wanatumia Unga wa Muhogo kwa muda wote na kushindwa
kuchangia ipasavyo chakula mashuleni kwani wanatakiwa kupeleka Mahindi na
Maharage
Kwa upande
wake Afisa mtendaji wa kijiji cha Kumuhasha Bi Joyce Simon alipoulizwa alikili kuwepo kwa tatizo
hilo na kusema kuwa kingine kilichochangia ni baadhi ya wakulima kuchelewa
kuandaa mashamba kwa wakati kwenye mvua za mwanzo
Hata hivyo
Bi Joyce aliongeza kuwa kulingana na hali hiyo uongozi wa kijiji unafaya
jitihada kutoa elimu ili wananchi waweze kulima mazao yanayovumilia ukame kisha
watajaribu kulipeleka swala hilo, katika ngazi ya wilaya kwa msaada zaidi na
kuwatakla wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu bila utaratibu kwani hali
hiyo uchangia mabadiliko ya hali ya hewa, kuleta jangwa na mvua kukosekana
Maoni
Chapisha Maoni