Mgombea uraisi kupitia chama cha ukombozi wa umma Chauma Bw.Hashimu Rungwe amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka huu atahakikisha anasimamia Elimu ya watu wazima na kilimo ndege ndiyozitakazomwagilia mashamba ya wakulima .


Hashim Rungwe nikiwa Rais ndege zitamwagilia mashamba ya wakulima


Mgombea uraisi kupitia chama cha ukombozi wa umma Chauma Bw.Hashimu Rungwe amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka huu atahakikisha anasimamia Elimu ya watu wazima na kilimo ndege ndiyozitakazomwagilia mashamba ya wakulima .

Hayo aliyasema jana wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika wilaya ya kibondo mkoani kigoma alipokuwa akiomba kura kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la mhambwe kupitia chama hicho  Bw.Nduhirubhusa mapigano.

Bw.Rungwe amesema jamii  kubwa katika nchii hii inakabiliwa na matatizo ya matabaka ya walionacho na maskini hali inayosababisha chuki na kueleza kuwa yeye atamwezesha kila mwenye uwezo wa kufanya kazi kupata fulsa nzuri hasa kutoa elimu katika kile wanachowezakukifanya ili kuleta maendeleo kwa wote na kuondoa matabaka

Aliongeza kuwa ni vema kuwa kila mmoja akafanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato cha familia na kuleta maendeleo kwani serikali kazi yake ni kumboreshea mwananchi mazingira ya kufanya kazi kama kuboresha elimu afya na na mambo yanayostaili

Aidha alisema kuwa mambo yote anayoyasema yanawezekana kwani Tanzania inazo fursa za kuwezesha yote hayo tatizo lililopo ni baadhi ya watu kutaka kujinufaisha wao peke yao na kuyaacha makundi makubwa yakiishi kwa umasikini hatua inayosababisha chuki miongoni mwa watanzania
K
wa upande wake mgombea mwenza kutoka visiwani Zanzibar Bw.Issa Husein amesema chama cha ukombozi wa umma kina lengo lakutetea haki za wananchi katika kupunguza changamoto zinazo wakabili kwa kipindi kirefu ikiwemo na ukosefu wa miundombinu mibovu hususa  barabara na kufanya maisha ya mtanzania kuwa na ubora ikiwa ni pamoja na kudumisha muungano

Bw.Kayungu kabtari ni makamu mwenyekiti wa chama hicho taifa yeye amewataka watanzania kuhudhulia katika mikutano ya siasa ili kuwasikiliza juu sera zao na kuwapima kama wanafaa na kuondokana na dhana kuwa wapo wagombea harali na mabao hawastaili kwani wote ni sawa hakuna mwenye hati miliki ya kuongoza

Nduhirubhusa mapigano ambaye ni  mgombea ubunge kupitia chama hicho jimbo la muhambwe wakati alipopewa nafasi ya kura, alisema kuwa katika wilaya kibondo hakuna Gari la kuzimia moto hali inayowafanya kuishi kwa hofu ila akipewa nafasi ya kuongoza atalishugulikia tatizo hilo kwa kushirikiana na Halmashauri

Hashim Rungwe mgombea urais kupitia chama cha ukombozi wa umma
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambapo mmoja wao James Jovin wagombea  mbalimbali wa nafasi za urais ubunge na udiwani kuhakikisha wanaahidi mambo yanayowezekana ili kuondoa mkanganyiko baadae na kuondoa imani kwa serikali
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji