Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

Walimu wa shule za msingi na sekondari kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha alimu wilayani Kibondo mkoani Kigoma jana walisimamisha shuguli za ufundishaji katika shule zao na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo ili kudai stahiki zao ikimwemo upandishwaji wa madaraja

Picha
Judathadius mboya Ded Kibondo Lyaki Majo mwenyekiti cwt Kibondo Walimu wa shule za msingi na sekondari kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha alimu wilayani Kibondo mkoani Kigoma jana walisimamisha shuguli za ufundishaji katika shule zao na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo ili kudai stahiki zao ikimwemo upandishwaji wa madaraja Walisema licha ya serikali kutoa waraka wa mwongozo kuwa walimu wote ambao ngazi zao zimefikia mwisho, wapandishwe madaraja, kakini  kumekuwepo na matatizo ambayo yamekuwa yakisababishwa na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuto watendea haki Wakiongea kwa jaziba na wengine kuangua vilio katika mkusanyiko huo walieleza pamoja na kufuatilia mara kwa mara ili wapate hatima ya madai mbalimbali bila mafanikio huku wakipewa majibu ya kukatisha tamaa kwa kuambiwa huku wengine kati yao wakilipwa fedha nusu na wengine wakiambulia patupu alisema Rashidi Mlaki  nakuongeza kuwa sababu ni watumishi waliochin...

Mwanaume Furaha John, mkazi wa kijiji cha Kinonko wilaya ya Kakonko mkoani alieyejikata utumbo kwa wembe na kulazwa katika Hospitali ya wilaya Kibondo hali yake imeendelea kuimarika kutokana na na jitihada za madaktari kuendelea kumpa matibabu

Mwanaume Furaha John, mkazi wa kijiji cha Kinonko wilaya ya Kakonko mkoani alieyejikata utumbo kwa wembe na kulazwa katika  Hospitali ya wilaya Kibondo hali  yake imeendelea kuimarika kutokana na na jitihada za madaktari kuendelea kumpa matibabu Kwa mujibu wa maelezo yake amesema  hali yake ya afya inaendelea vizuri baada kufanyiwa upasuaji na kupata matibabu maana alipofikishwa hospitalini hapo fahamu zake hazikuwa sawa kutokana na maumivu aliyokuwanayo, ila hivi sasa anaendelea vizuri maana anaweza kula,  na kutembea pia. Hata hivyo amesema  kutokana  na matatizo aliyokutana nayo atalazimika kuachana kunywa  na kufanya biashara ya kutengeneza pombe za kienyeji maana uenda ndo zimemsababishia matatizo na ameamua kumrudia Mungu wake Hamis Mohamed ambae ni muuguzi katika wod alimolazwa Furaha, anasema hivi sasa mgonjwa huyo anaendelea vizuri tofauti na alivyofikishwa  hospitalini hapo Kwa upande wake Daktari ambae amekuwa akimtibu,...

Zoezi la kumkataa katibu wa Ccm wilaya Kibondo Kigoma Hamis Kananda limechukua sura mpya Baada ya uongozi wa chama hicho mkoa, kuunda tume kwa ajili ya kuwahobi wajumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya juu ya tuhuma zinazosukumiwa kwa katibu wao na kuamuru aachie ngazi

  Zoezi la kumkataa katibu wa Ccm wilaya Kibondo Kigoma Hamis Kananda limechukua sura mpya Baada ya uongozi wa chama hicho mkoa, kuunda tume kwa ajili ya kuwahobi wajumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya juu ya tuhuma zinazosukumiwa kwa katibu wao na kuamuru aachie ngazi Taarifa za ndani za  kikao cha halmashauri ya ccm wilaya kilichofanyika mjini kibondo jumatatu wiki hii,kwa kushirikiana na wajumbe  wa tume hiyo, iliyoongozwa na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Kigoma Bw, Aman Kaburu  kwa ajili ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili Hamis Kananda, baada ya kuhoji  pande zote mbili,zinaeleza  kuwa katibu huyo alitumia vibaya madaraka yake kwa kukiuka taratibu na kukihujumu chama hicho Kutokana na jazba walizokuwa nazo wajumbe wa kikao hicho awali viongozi wa ambao ni kalembe Masod, katibu mwenezi Mkoa, walijitahidi kuwatuliza  ili mkutano uweze kwenda kwa amani na utulivu ili lengo linalokusudiwa liweze kupatikana    Kwa mujibu wa maelezo...