Mwanaume Furaha John, mkazi wa kijiji cha Kinonko wilaya ya Kakonko mkoani alieyejikata utumbo kwa wembe na kulazwa katika Hospitali ya wilaya Kibondo hali yake imeendelea kuimarika kutokana na na jitihada za madaktari kuendelea kumpa matibabu
Mwanaume Furaha John, mkazi wa kijiji cha Kinonko wilaya ya
Kakonko mkoani alieyejikata utumbo kwa wembe na kulazwa katika Hospitali ya wilaya Kibondo hali yake imeendelea kuimarika kutokana na na
jitihada za madaktari kuendelea kumpa matibabu
Kwa mujibu wa maelezo
yake amesema hali yake ya afya inaendelea
vizuri baada kufanyiwa upasuaji na kupata matibabu maana alipofikishwa
hospitalini hapo fahamu zake hazikuwa sawa kutokana na maumivu aliyokuwanayo,
ila hivi sasa anaendelea vizuri maana anaweza kula, na kutembea pia.
Hata hivyo amesema kutokana na matatizo aliyokutana nayo atalazimika
kuachana kunywa na kufanya biashara ya
kutengeneza pombe za kienyeji maana uenda ndo zimemsababishia matatizo na
ameamua kumrudia Mungu wake
Hamis Mohamed ambae ni muuguzi katika wod alimolazwa Furaha,
anasema hivi sasa mgonjwa huyo anaendelea vizuri tofauti na alivyofikishwa hospitalini hapo
Kwa upande wake Daktari ambae amekuwa akimtibu, Dr Adam
Jonathan, amesema uenda akaruhusiwa muda wowote kwa kuwa hali yake imeanza
kuridhisha, katika swala la kitaalam Adam amesema uenda Mtu huyo akapata tatizo
la mmeng’enyo wa chakula sababu kazi hiyo ufanywa na utumbo na sasa umepungua
baada ya kuondolewa
Kwa upande wake John Nkonkoili ambaye ni Baba mzazi wa Kijana huyo,
na ambaye anamuuguza, katika maelezo yake amesema kuwa yeye Ndugu na jamaa walishangazwa na uamuzi aliouchukua ndugu yao wa kuamua kujiua kwa kijiumiza kiasi hicho, tena kwa kuonyesha
ujasili mkubwa na kuongeza kuwa watakaa pamoja ili wajadili na kumpa ushauri
ili jambo hilo lisijirudie tena
Awali Mwanaume huyo Feb 29 mwaka huu,katika kijijini cha Kinonko, wilaya ya kakonko,
alijikata Tumbo lake na kisha kuumwaga utumbo wake nje na kuanza kuukata
vipande ili ajiue, baada ya kufanya jaribio la kujinyonga kwa kamba kwa madai
ya Kudhulumiwa kiasi cha Tsh 35,000/ na mfanyabiashara mwenzake na baada ya
kufika nyumbani kwake kunyimwa chakula na mke wake
Maoni
Chapisha Maoni