Walimu wa shule za msingi na sekondari kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha alimu wilayani Kibondo mkoani Kigoma jana walisimamisha shuguli za ufundishaji katika shule zao na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo ili kudai stahiki zao ikimwemo upandishwaji wa madaraja


Judathadius mboya Ded Kibondo

Lyaki Majo mwenyekiti cwt Kibondo



Walimu wa shule za msingi na sekondari kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha alimu wilayani Kibondo mkoani Kigoma jana walisimamisha shuguli za ufundishaji katika shule zao na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo ili kudai stahiki zao ikimwemo upandishwaji wa madaraja

Walisema licha ya serikali kutoa waraka wa mwongozo kuwa walimu wote ambao ngazi zao zimefikia mwisho, wapandishwe madaraja, kakini  kumekuwepo na matatizo ambayo yamekuwa yakisababishwa na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuto watendea haki

Wakiongea kwa jaziba na wengine kuangua vilio katika mkusanyiko huo walieleza pamoja na kufuatilia mara kwa mara ili wapate hatima ya madai mbalimbali bila mafanikio huku wakipewa majibu ya kukatisha tamaa kwa kuambiwa huku wengine kati yao wakilipwa fedha nusu na wengine wakiambulia patupu alisema Rashidi Mlaki  nakuongeza kuwa sababu ni watumishi waliochini ya Mkurugenzi

Hatua hiyo waliitaja kuwa ni ya kulipa kwa ubaguzi tena kwa upendeleo, inaashilia kuwepo kwa mianya ya rushwa kwa watendaji hao wa halmashauri hiyo na kuiomba serikali ingilie kati ili wapate haki zao kwani halmashauri zingine zimesha wakamilishia stahiki watumishi wao kwa kupanda madaraja na malipo mengine

Judathadeus Mboya ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo halipata wakati mgumu katika kuwapa majibu walimu akiwaeleza kuwa tatizo lilikuwa ni kwenye mfumo majina ya walimu katika bajeti ili waweze kupanda madaraja maelezo ambayo hayakukubaliwa.

Kutokana na hali hiyo ya kutoelewana mkurugenzi huyo alisema maelezo ya kukwama kwa upandishwaji wa walimu madaraja, alipewa na maafisa utumishi wake na hakuridhika nayo na anatarajia kuchukua hatua za kinidhamu kwa waliohusika ila wawe na subila wakati taratibu zikifanyika

Hata hivyo Kaimu Afisa utumishi wa halmashauri hiyo, Bw, Staford Herman amesema kuwa kuwa majina ya walimu 66 yalisahalika tu kimakosa lakini hata wao hausiki na upandishaji madaraja bali afisa utumishi mkuu kupitia hazina ndiyo wahusika wakuu

Walimu wanaotakiwa kupandishwa madaraja kutoka E kwenda F ni264 na kutoka F kwenda G 22 H kwendaI ni 2 jumla yao ni 288na wanaopanda kwa mtiririko kuta daraja B kwenda C ni 72  huku upande wa sekondari kutoka C kwenda D 13na kutoka D kwenda E walimu14E kwenda F 1na kutoka Fkwenda G ni 1 jumla ya wote ni 389

Tamko la chama cha walimu wilayani kibondo likitolewa na Katibu wake Bw, Lyaki Majo, lisema kwakuwa waathilika ni 389 idadi ambayo ni kubwa sana, wanatoa siku 14 na kwa mkurugenzi kuhakikisha anarekebisha madai yote ya walimu na kuwapandisha madaraja wale wote wanapaswa kufanyiwa hivyo na kama ufumbuzi hautakuwepo wataanzisha mgomo usiokuwa na kikomo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji