Zoezi la kumkataa katibu wa Ccm wilaya Kibondo Kigoma Hamis Kananda limechukua sura mpya Baada ya uongozi wa chama hicho mkoa, kuunda tume kwa ajili ya kuwahobi wajumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya juu ya tuhuma zinazosukumiwa kwa katibu wao na kuamuru aachie ngazi
Zoezi la kumkataa katibu wa Ccm wilaya
Kibondo Kigoma Hamis Kananda limechukua sura mpya Baada ya uongozi wa chama
hicho mkoa, kuunda tume kwa ajili ya kuwahobi wajumbe wa Kamati ya siasa ya
wilaya juu ya tuhuma zinazosukumiwa kwa katibu wao na kuamuru aachie ngazi
Taarifa za ndani za
kikao cha halmashauri ya ccm wilaya kilichofanyika mjini kibondo
jumatatu wiki hii,kwa kushirikiana na wajumbe wa tume hiyo, iliyoongozwa na mwenyekiti wa
ccm mkoa wa Kigoma Bw, Aman Kaburu kwa
ajili ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili Hamis Kananda, baada ya kuhoji pande zote mbili,zinaeleza kuwa katibu huyo alitumia vibaya madaraka
yake kwa kukiuka taratibu na kukihujumu chama hicho
Kutokana na jazba walizokuwa nazo wajumbe wa kikao hicho
awali viongozi wa ambao ni kalembe Masod, katibu mwenezi Mkoa, walijitahidi
kuwatuliza ili mkutano uweze kwenda kwa
amani na utulivu ili lengo linalokusudiwa liweze kupatikana
Kwa mujibu wa maelezo ya katibu mwenezi wa ccm wilaya hiyo, Hamisi Tairo, alipokuwa akihojiwa na na Gazeti hi, alisema kuwa Katibu huyo wa Ccm wilaya ya kibondo Bw,
Hamis Kananda, anatuhumiwa kuhujumu mali za chama hicho, ikiwemo fedha zaidi
shilingi milion 77 milion 10 kwa ajili kujenga wod hospitalini na milion 67 za
posho za mabalozi tawi na vijiji
Aidha lisema kuwa
baada ya uongozi mkoa wa kigoma kupitia taratibu zote za vikao na kubaini
matatizo yote, , hivyo kuonekana kuwa
katibu kananda si mwaminifu, kikao hicho kilitoa maamuzi kuwa katibu huyo
Hamas Kananda, kusimama kazi au kuhamishiwa kituo kinginge.
Baadhi ya wajumbe waliokuwa kwenye kikao hicho cha
halmashauri kuu ya ccm wilaya ambao ni Tatu Barakabise na Ayub Mnyiriri, jana waliutaka uongozi wa juu kutatua migogoro
kwani inasababisha watu kioamini chama na baadae kuleta migongano huku
wakimtaka katibu huyo kwakuwa amebainika alipe fedha alizopoteza
Kwa upande katibu huyo anayelaumiwa alipouliza juu ya tuhuma
hizo zinazozidi kuongezeka amesema kuwa yeye hajaiba pesa yoyo na alishahojiwa
na tume hiyo kwenye kamati ya siasa ya wilaya alikuwa anasubiri kukaguliwa kwa
mujibu wa taratibu za kifedha, na fedha zote za mabarozi anazotuhumiwa kuiba
aliwalipa kwa mujibu wa Taratibu na nakala zipo zinaonyesha wazi
Aliongeza kuwa halmashauri haikutakiwa kujadili swala hilo bila kuomba zinazoonyesha malipo
jinsi yalivyofanyika na kueleza kuwa kamati hiyo niya kisiasa na mgogoro huwo
unatengezwa na mtu ili kumchafua kuhusu kuenguliwa kwake amesema yeye bado
hajapata barua ya kumsimamisha kazi wala kuhama na ni katibu halali wa ccm
Wilaya ya kibondo
Ikumbukwe kuwa mnamo 16 feb mwaka huu kiliitishwa kikao cha
halmashauri kuu wa wilaya kwa ajili ya kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu
uliofanyika 25 octoba 2015 ulivyoenda
badala yake kibao kilimgeukia katibu huyo baada ya wajumbe kutaka isijadiliwe
agenda yoyote mpaka katibu wa ccm wa wilaya hiyo aleze upotevu wa shiling 10
milion za chama hicho, hali ilizua mtafaluku na kikao kuvunjika na kupelekea
uongozi wa mkoa kuingilia kati
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni