Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini
Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini Akiongea na Wananchi wa Mikoa hiyo jana, George Mbijima ambaye ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2016 kwenye makabidhiano ya Mwenge wa uhuru uliokuwa ukitoka Kigoma na kwenda Kagera, amewataka wakazi wa mikoa hiyo wanapoona kuwa kuna wimbi la watu hao watoe taarifa kwa viongozi ili hatua zichukuliwe Aidha Mbijima alisema kuwa wapo baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakishirikiana na wahamiaji haramu kwa kufanya vitendo vya uharifu wa kutumia siraha kama ujambazi na ujangili hali ambayo imekuwa ikisababisha mauwaji ya raia wasiyokuwa na hatiana kirudisha nyuma maendeleo ya watu ‘’Serikali haitalifumbia macho jambo hili na mtu yeyote atakaebainika kuwakumbatia...