Watendaji katika Idara mbalimbali za halmasauri za wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata miongozo taratibu za kazi na kutumia taalumao ili kuleta ufanisi na kuondoa manug’uniko katika jam

Kibondo;

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Luis Peter Bule akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kasulu ulipokuwa ukianza mbio zake wilayani kibondo





Watendaji katika Idara mbalimbali za halmasauri za wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata miongozo taratibu za kazi na kutumia taalumao ili kuleta ufanisi na kuondoa manug’uniko katika jamii

Kauli hiyo ilitolewa jana  na Kiongozi wa mbio za mwenge  Kitaifa George Mbijima alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kibondo Mkoani kigoma mwenge huo ulipofanya mbio zake wilayani humu kama taratibu zambio  zake zinazoendelea  hapa nchini

Mbijima ameseme kuwa hivi sasa serikali imeelekeza nguvu zake wanawake na Vijana katika kuwawezesha kwa kupitia katika halmashauri zao lakini wapo baadhi ya watendaji wasiokuwa waadilifu mara zinapotokea fulsa kwa walengwa wao uzipora na kuwapa watu wao au kuziingiza katika makampuni yao binafsi

Mwenge  huo katika mbio zake wilayani Kibondo  ulitembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya million mia 960,961,775 na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujiepusha na matumiszi ya madawa ya kulevya , Maambukizi ya ukimwi, na kutoa hamasa kwa vijana wanawake kujunga na kufanya kazi iliweze  kuongeza kipato  cha familia ambapo kiongozi huyo amewataka vijana kushiriki katika kazi na kuheshimu utu wao  waweze kuthaminiwa ndani ya jamii ndipo na shirikishwaji utakapo kuwepo

‘’Vijana kutokana na mienendo yetu mibaya tunasomeka katika jamii kuwa ni wathuni ambao hatusitahili kushirikishwa katika mambo mbalimbali ya kijamii na kifamilia lakini tukijiheshimu kwa kufuata maadili hata ushirikishwaji utakuwa na maana  alisema Mbijima kiongozi mbio za Mwenge 2016’’

Kwa upande wao baadhi ya wanawake katika vikundi vyao waliotembelewa wameiomba serikali pamoja na kuweka mkazo kuwajali wanawake na Vijana  kwa kutaka kuwawezesha walisema lakini  wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya ujasiliamali huku vijana ambao ni Josephat Kanguye na Rodah Linus, wakipongeza uhamasishaji unaotolewa kujiepusha na madawa ya kulevya

Katika kujibu maombi ya wanawake hao Mbijima ameitaka halmashauri ya wilaya ya kibondo kuhakikisha inatoa elimu kwa makundi hayo ili yaweze kufanya kazi  ipasavyo ambapo Kaimu Murugenzi wa halmashauri hiyo Said Shemahonge ameahidi baada ya wiki mbili wataanza kutoa elimu hiyo
Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Wazazi timizeni wajibu wenu katika Malezi ili Watoto wenu wafikie Ndoto zao