Kibondo; Serikali ya Uberigiji kupitia shiraka la Maendeleo la nchini humo BTC, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania imetoa msahada wa Mahema 22 yenya thamani ya shilingi milion miamoja kwa ajili ya wakulima na wafugaji Nyuki wa Mkoa wa kigoma ili kuboresha utendaji kazi wakati wa uvunaji wa mazao ya nyuki
Mwemezi Muhingo Mwananchi
Kibondo; Serikali ya Uberigiji kupitia shiraka la Maendeleo la nchini humo BTC, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania imetoa msahada wa Mahema 22 yenya thamani ya shilingi milion miamoja kwa ajili ya wakulima na wafugaji Nyuki wa Mkoa wa kigoma ili kuboresha utendaji kazi wakati wa uvunaji wa mazao ya nyuki
Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi mahema hayo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kigoma Kaimu katibu Tawala wa mkoa huo anaehusika na ushauri wa uchumi Robinson Mwanjala ambae alikuwa mgeni rasmi, ameipongeza serikali ya uberigiji wakati wa kukabidhi msahada huo na amewataka wafugaji nyuki kuhakikisha wanayatumia ipasavyo na kwa malengo yanayo kusudiwa ili kazi yao iweze kuwa na tija
Mwanjala aliwataka wafugaji hao na wakulima kuhakikisha wanatumia vizuri elimu waliopewa katika kuvuna mazao ya Nyuki kwa kuzingatia usalama wa chakula kwa watumiaji ambapo vikundi 7 vya ushirika katika wilaya za kakonko KibondoUvinza, Kasulu na Buhigwe vilinufaika na msahada huo
''Kumewepo na na Tabia za baadhi ya watanzania kutokujali misahada inayotolewa na wahisani kwa kuharibu hata miundo mbinu wanayopewa hali inayopelekea watu hao kukata tamaa ya kutaka kuendelea kusaidia, hivyo tunzeni mahema haya kwani ni faida kwenu wenyewe alisema mwanjala .
Hata hivyo Afisa mazingira wa wilaya kibondo Mohamed Semdoe katika taarifa yake alisema kuwa wafugaji nyuki na wakulima katika maeneo mengi ya mkoa wa kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kutokuwepo na kwamipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji na mapori pamoja taasisi nyingi za kifedha kutotoa mikopo kwa wafugaji kwa madai hawana sifa za kukopesheka hali inayopekelea uzalishaji dumi kwa wakulima na wafugaji
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi shirika la maendeleo la Uberigiji BTC Thomi Smith, ameishukuru serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na utalii hapa nchini kwa kuruhusu wafuga nyuki kufanyaka zi zao katika mapori ya hifadhi ya wanyama na kongeza kuwa mahema hayo yatapunguza usumbufu kwa walengwa na kupata mazao yenye viwango vinavyokubalika
Nao baadhi ya wafugaji ambao ni Abubakali Chiizerona Paulina Meshack, walisema hapo awali walikuwa wakifanya shughuli zao kwa usumbufu mkubwa mara wanapokwenda kuvuna asali maporini ambapo wamekuwa wakikosa sehemu ya kutunzia bidhaa zao wakilala chini ya miti huku wakipoteza mizigo yao na wakikabiliwa na hatari ya kushambuliwa na wanyama wakali na baada ya kupewa mahema hayo yatasaidia kutunzia mazao ya nyuki na kuweka bidha hizo katika hali ya usalama wakisubiri kusafirisha majumbani mwao
Seif Salum ambae ni mratibu wa kitengo cha nyuki katika halmashauri ya wilaya kibondo shirika la BTC alisema kuwa wafugaji nyuki wengi katika mkoa wa kigoma wamekuwa wakipata shida kubwa wanapokwenda kuvuna asali na kukosa jinsi ya kuhifadhi hali ambayo ingepelekea kupatikana kwa mazao ya nyuki yasiyokuwa viawango vinavyokubalika na baadae kushuka bei katika masoko hivyo mahema hayoyatasaidia kuzuia asali kujaa maji na hema moja wanaweza kulala watu 30
Maoni
Chapisha Maoni