Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini
Wakazi wa mikoa ya Kagera na Kigoma ambao mikoa yao iko mipakani mwa Nchi za Burundi na Rwanda wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria ambapo wengi wao wamekuwa wakiingia na siraha za Mototo na kuzitumia katika uharifu hapa nchini
Akiongea na Wananchi wa Mikoa hiyo jana, George Mbijima ambaye ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2016 kwenye makabidhiano ya Mwenge wa uhuru uliokuwa ukitoka Kigoma na kwenda Kagera, amewataka wakazi wa mikoa hiyo wanapoona kuwa kuna wimbi la watu hao watoe taarifa kwa viongozi ili hatua zichukuliwe
Aidha Mbijima alisema kuwa wapo baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakishirikiana na wahamiaji haramu kwa kufanya vitendo vya uharifu wa kutumia siraha kama ujambazi na ujangili hali ambayo imekuwa ikisababisha mauwaji ya raia wasiyokuwa na hatiana kirudisha nyuma maendeleo ya watu
‘’Serikali haitalifumbia macho jambo hili na mtu yeyote atakaebainika kuwakumbatia wahamiaji haramu na kushirikiana nao kufanya uharifu atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali hivyo lazima kila Mtu awe mlinzi wa mwenzake lazima tulinde amani ya nchi yetu na tusikubali ikavulugwa na watu wasiokuwa waadilifu alisema Mbijima’’
Pamoja na mambo mengine wakati wamakabidhiano hayo yaliyofanyika Kwenye kijiji cha Murusagamba Wilayani Ngara Mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia General mstaafu, Emmanuel Maganga, alisema kuwa mwenge huo ulipo kuwa mkoani kwake ulitembelalea miradi 52 yenye thamani tsh Bilion 15 na kutoa elimu kwa wananchi na yeye kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa wakati huo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Salum Kijuhu baada ya kukabidhiwa mwenge huo toka mkoani Kigoma, amesema kuwa Mwenge utakapokuwa kwenye eneo lake, utatembelea, kukagua, Kuzindua na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi 62 yenye Thamani ya Tsh Bilion 17
Maoni
Chapisha Maoni