Mashabiki wa Simba waadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii
Vaileti Macha Mwanafunzi shule ya sekondari Kibondo |
Frolrntina Thelathini Mwanafunzi |
Hija Othman Mwenyekiti wa Simba Tawi la Kibondo alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari |
Hija Othman Mwenyekiti wa Club ya Simba Tawi la Kibondo alipokuwa akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kibondo |
Kuelekea Kilele cha maadhimisho siku ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba Wanachama na Mashabiki wa Timu hiyo Wilayani Kibondo Kigoma, leo Agost 5,2023 wametoa Msaada wa Taulo za Kike kwa wanafunzi wa shule ya sekkondari ya wasichana Kibondo
Hija Othman ni Mwenyekiti wa Tawi la Kibondo ameeleza lengo na madhumuni ya kutoa msaada huo kuwa kwa kile wanachokipata ni lazima kirudishwe kwenye Jamii
Aidha amesema kuwa kuwa Watoto wa Kike hasa walioko mashuleni wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kupata vifaa vya kujistili wakati wa hedhi hatua ambayo upelekea kuathirika kisaikolojia ka kushusha kiwango cha ujifunzaji
Licha ya utoaji wa Msaada ya Taulo za Kike Wapenzi,Mashabiki wa Timu Simba walifanya usafi katika Kituo cha Afya cha Kibondo Mjini na kupanda Miti kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira na siku ya Jumapili Agosti 6,2023 watashiriki katika zoezi la uchangiaji Damu litakalofanyika katika Jumba la maendeleo Kibondo Mjini ambapo ndiyo siku ya Kilele cha Tamasha la Siku ya Simba
Nao baadhi ya Wanafunzi waliopatiwa msaada huo ambao ni Frolentina Thelathini na Vaileti Macha wametoa shukrani kwa wanachama wa Club hiyo ya Simba wamesema Msaada huo wa Taulo za Kike zitapunguza changamoto za kukosa vifaa hivyo na kueleza kuwa wanapokuwa wamekosa mahitaji hayo uathirika kwa kutojifunza ipasavyo pia msaada huo utasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili
Maoni
Chapisha Maoni