KIBONDO KUUNDA SHERIA NDOGO KATIKA UCHANGIAJI WA CHAKULA MASHULENI
Gabriel Chitupila Kaimu Mkurugenzi Hshauri Kibondo Jacklin Sospeter Afisa Lishe wilaya ya Kibondo Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Kamati ya Lishe wilayani Kibondo waliokuwa wakitathmin hali ya Lishe wilayani Kibondo KIBONDO KUUNDA SHERIA NDOGO KATIKA UCHANGIAJI WA CHAKULA MASHULENI Licha ya hamasa na elimu kuendelea kutolewa kwa jamii juu ya uuchangiaji chakula mashuleni ili wanafunzi wapate chakula cha mchana Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, hatua hiyo bado ni kizungumkuti kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kutoa michango ya chakula na wanafunzi kushinda njaa Baadhi ya wanafunzi wanapata chakula cha mchana na uji saa nne kutokana na wazazi wao kuchangia huku wengine wakishinda njaa mashuleni kutokana na wazazi na walezi kushindwa kutoa michango ya chakula Wanafunzi akiwemo Abdukarim Ramadhani na Jesca Reuben chakula wala uji ambao hawapati wamesema wanakumbana na wakati mgumu mara inapofika nyakati za mchana kutoka na kuhisi njaa ambapo usinzia na kus...