CHANGAMOTO WANAFUNZI WANAOACHA SHULE
Muhingo Mwemezi Kigoma
Kigoma. Licha ya uwepo wa maendeleo ya
upatikanaji wa Elimu hapa nchini katika shule za Msingi na sekondari bado tatizo la Wanafunzi kushindwa kumaliza
shule ni kubwa na linaendelea kutokana
na saababu mbalimbali na kupelekea Watoto kukosa haki za Msingi
Changamoto
hiyo haina budi kutiliwa mkazo ikiwa ni pamoja na jamii Wazazi na Walezi kote nchini kuendelea
kuhimizwa na kuelimishwa kutambua umuhimu wa Elimu, ambapo makundi ya rika
barehe kuanzia miaka 9 hadi 15 ndiyo wahanga wakubwa
Tatizo hilo
linachangiwa na sababu mbalimbali kama Umasikini Umbali wa kutoka katika maeneo
ya Makazi kwenda kwenye huduma za shule hatua ambayo hupelekea Watoto wengi
kukata tamaa wakati mwingine kukumbwa na
Vitendo kikatili mfano Takwimu za mwaka 2022 Mkoa wa Kigoma ulipata nafasi ya 8
Takwimu hizo
zinaonyesha Mkoa huo una Watoto
waliokatisha masomo 10,355 wa shule za
Msingi na ulikuwa wa na 17
kwa kuwa na Idadi ya Wanafunzi 4,231kwa shule za Sekondari
Hali hiyo
iliweza kuwaibua Wadau wa Elimu Plan Internation kupitia Mradi Kagis [ Keeping
Adolescent Girls in School] kusaidia Makundi ya Wasichana ambao wanaishi katika
mazingira magumu na wanatembea mwendo mrefu kwenda shule kwa kuwapatia Baiskeli
katika Halmashauri ya Geita na Geita Mji
Mkoani Geita na Kibondo Mkoani Kigoma
Nikodemas Gacho Mkuu wa Mradi wa Kagis alipokuwa kwenye Uzinduzi wa utoaji wa
Baiskeli kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Biturana Kibondo Mkoani
Kigoma alisema hadi kukamilika kwa mradi
huo wanatarajia kutoa Baiskeli 2200 ambapo mwaka jana zilitolewa Baiskeli 550
Geita, na mwaka huu zilizotolewa ni ni 300 kwa Geita na 259 wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
Hata hivyo
Nikodemas ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa serikali na Mashirika kuungana kwa pamoja kukwamu makundi haya
ambayo yanakumbwa na masibu mbalimbali hasa wasichana
Afisa Elimu
Mkoa wa Kigoma Simon katika shukrani zake Shija akiwataka viongozi kuhamasisja
jamii juu ya umuhimu wa elimu na kuwataka wananchi kutambua kuwa Wahisani mara
nyingi wana muda maalu wa kuendelea kutoa misaada hivyo ni vema kujipanga namna
ya kundeleza Watoto hao, huku Rasta
Bally toka ubalozi wa Canada akisema
wanashirikiana na Tanzania kuboresha Elimu ya Mtoto wa Kike na kuwahasa
Wanafunzi hao kupenda elimu kwani ndiyo urithi wao
Asha Isaya
na Mariam Lameck ni baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Biturana
wameeleza adha wazokutana nazo ktembea mwendo mrefu wanafika shuleni
wamechelewa na kuadhibiwa na walimu na wanaporudi majumbani mwao ushindwa kuendela na shughuli zingine huku
Mratibu Elimu Kata ya Biturana Benard
Shibabo akisema kuwanafunzi katika kata yake wanatembea ubali wa kilomita 7
hadi9 na kuongeza kuwa kwa mwaka jana wanafunzi waliacha shule za msingi ni 50
na 30 sekondari
Nae Mkuu wa
Wilaya ya Kibondo Kanali Aggrey Magwaza aliyewakilishwa na Katibu Tarafa ya
Kifura, Omary Shekarata ameitaka jamii kuthami Misaada inayotolewa na Wahisani
na kueleza Baiskeli hizo zisitumiwe na watu wazima zitunzwe Mwanafunzi
anapomaliza elimu yake anarudisha Baiskeli hiyo shule ili watumie wengine
Mradi wa
Kagis katika Shirika la Plan Intertion unafadhiliwa na Serkali ya Watu wa
Canada na unalenga kuwafikia
wanufaika102,236 ambao wanafunzi ni 96, wasichana 49,336 wavulana 47,162 wenye
umri wa miaka 9 hadi 15 katika shule za Msingi 73 na sekondari 17 na walio nje ya shule 5,900 wasichana na 2, 950 katika Vijiji 118
Maoni
Chapisha Maoni