VIJANA JIAMININI NA MUWE NA MOYO WA KUFANYA KAZI
Meja Generali Hawa Kodi aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi Kikosini Kanembwa |
Luteni Kanali Mantange Kombe Kamanda Kikosi 824 Kanembwa |
Kanali Evance Malasa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mgeni rasmi |
Janeth Alex Mmoja wa Wahitimu mafunzo ya awali ya Kijeshi Kanembwa |
Kakonko. Vijana wametakiwa kujiamini na kuwa na moyo
wa kupenda kufanya kazi na kuwa tayari kulitumikia Taifa ili kuwa na Taifa lenye
ustawi mzuri
Akiwahutubia Vijana waliokuwa wanahitimu Mafunzo ya awali ya
Kijeshi vijana wa kujitolea katika Jeshi la kujenga Taifa Kikosi cha 824
Kanembwa kilichoko Kakonko Mkoani Kigoma mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi katika
Mahafali hayo, Meja Generali Hawa Kodi amesema Vijana ni Taifa la leo na kesho hivyo wana wajibu wa kujituma na kuheshimu
maamuzi yao na kuzingatia Nidhamu
Adha ameongeza kuwa Vijana katika kujiunga na Jeshi la kujenga
Taifa, walitoka kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na elimu,Makabila,Malezi na
uelewa tofauti hivyo Serikali kupitia Jeshi imetumia Garama kubwa kuelimisha na
kuwataka kuzingatia yale waliyofundishwa na kuyatendea kazi
Luteni Kanali Mantange
Kombe ambaye ni Kamanda Kikosi 824 Kanembwa KJ amesema Vijana hao watika
mafunzo licha ya Masuala ya ulinzi ujasiriamali na Stadi za maisha waliweza
kujifunza kufanya mambo sahii,sehemu sahihi, kwa wakati sahihi kwani ndiyo Dira
ya Mafanikio katika maisha
Kutokana na mafunzo waliyoyapata yamewajenga kuwa na uzalendo
katika nchi yao, Utii na ukakamavu wa hali ya juu katika kulitumikia Taifa
Baadhi ya Vijana Janeth Alex na Melensiana Wiliam waliohitimu
mafunzo ya awali ya Kijeshi Oparation Miaka 60 ya Jkt 2024 katika shukrani zao,
wamesema wametambua Taifa zuri ujengwa na Vijana wenye utii na nidhamu na
kuahidi kudumu ndani ya maelekezo hayo siku zote kwa faida yao wenyewe na Jamii
nzima ya Tanzania
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kako Kanali Evance Malasa aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo amewahasa Vijana kutokubali kushawishiwa na kujiunga na makundi yasiyofaa kwani kufanya hivyo ni usaliti
Maoni
Chapisha Maoni