KIBONDO KUUNDA SHERIA NDOGO KATIKA UCHANGIAJI WA CHAKULA MASHULENI
Gabriel Chitupila Kaimu Mkurugenzi Hshauri Kibondo |
Jacklin Sospeter Afisa Lishe wilaya ya Kibondo |
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Kamati ya Lishe wilayani Kibondo waliokuwa wakitathmin hali ya Lishe wilayani Kibondo |
KIBONDO KUUNDA SHERIA NDOGO KATIKA UCHANGIAJI WA CHAKULA MASHULENI
Licha ya
hamasa na elimu kuendelea kutolewa kwa jamii juu ya uuchangiaji chakula
mashuleni ili wanafunzi wapate chakula cha mchana Wilayani Kibondo Mkoa wa
Kigoma, hatua hiyo bado ni kizungumkuti kutokana na baadhi ya wazazi na walezi
kushindwa kutoa michango ya chakula na wanafunzi kushinda njaa
Baadhi ya
wanafunzi wanapata chakula cha mchana na uji saa nne kutokana na wazazi wao kuchangia huku
wengine wakishinda njaa mashuleni kutokana na wazazi na walezi kushindwa kutoa
michango ya chakula
Wanafunzi akiwemo
Abdukarim Ramadhani na Jesca Reuben chakula wala uji ambao hawapati wamesema
wanakumbana na wakati mgumu mara inapofika nyakati za mchana kutoka na kuhisi
njaa ambapo usinzia na kushindwa kusikiliza Mwalimu huku wanaopata chakula
wakichekelea na kueleza kuwa kwa sasa ushiriki wao katika masomo ni mzuri
‘’Kwakweli
tunapata shida sana tupopata njaa huku wenzetu wakielekea kupata chakula wakati
mwingine wenzetu wanakula tukiwa tumewatazama maana tunatoka majumbani asubuhi
bila kula chochote na shuleni tunatoka muda umeenda sana majira ya saa kumi
jioni’’alisema Jesca mmoja wa Wanafunzi wasiopata chakula shuleni
Kutokana na hali hiyo serikali Wilayani Kibondo
inalenga kuweka sheria ndogo ambazo zitasaidia wazazi ambao hawachangii chakula
ili waweze kufanya hivyo kuondoa usumbufu kwa wanafunzi
Akiwa kwenye
kikao cha Kamati ya Lishe wilaya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibondo
Gabriel Chitupila amesema kwa sababu maelekezo yameshatolewa kwa wazazi na
walezi na wengi hawajawa tayari kutoa michango na Watoto wanashindaa ni vema
utaratibu wa sheria ndogo ukafanyiwa kazi ili kufikia malengo yanayokusudiwa
Kwa upande
wake Afisa Lishe wilaya hiyo Jacklin Sospeter amesema Katika shule za Msingi
95 ambazo hazitoi chakula ni na 5 pekee
na zile zinazotoa chakula ni wanafunzi wachache wanaopata huduma hiyo
Jacklini
ameongeza kuwa licha ya changamoto zilizopo kumekuwepo na mwamko kwa baadhi ya
wazazi katika utoaji wa chakula tofauti siku zilizopita kwani ahapo awali licha
ya elimu kutolewa wazazi wengi walikuwa wanagoma kabisa ila kwa sasa hali ni
tofauti ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita
Maoni
Chapisha Maoni