Sekta ya kilimo inayotajwa kama uti wa mgongo wa Taifa hili la Tanzania, na kuonekana kuwa ni muhimu sana tangu miaka ya nyuma, lakini hivi sasa umhimu huo umeanza umepotea baada ya wakulima na wafugaji kutotambulika ipasavyo kwa ajili ya kupata mahitaji ya lazima ili kuweka ubora kwa kile kinachotarajiwa
Bidhaa za mazo ya Nyuki |
Seif Salumkitengo cha ufugaji nyuki Kibondo |
Bw, Nuhu Kaali Meneja NMB Kibondo |
Abel Nyasio mfugaji nyuki |
Kibondo; Sekta ya kilimo inayotajwa kama uti wa mgongo wa Taifa
hili la Tanzania, na kuonekana kuwa ni muhimu
sana tangu miaka ya nyuma, lakini hivi sasa umhimu huo umeanza umepotea baada
ya wakulima na wafugaji kutotambulika ipasavyo kwa ajili ya kupata mahitaji ya
lazima ili kuweka ubora kwa kile kinachotarajiwa
Kukokesekana kwa hati miliki za
mali ambazo hazihamishiki kama mashamba na majumba maeneo ya vjiji kimekuwa
ndicho kikwazo kikubwa ikiwena ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya maswala ya
mikopo
Wakizungumzia swala hilo, jana
wakulima na wafugaji wakati wa uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushiri Kibondo
mkoani kigoma ambao ni Abeli Nyasio na Sospiter Eliya wamelalamikia hali inayowakumba ya
kutotambuliwa na taasisis za kifedha hapa nchini ili kupata huduma za mikopo
kwa madai hawana sifa za kukopesheka hatua inayowasababishia kutofikia malengo
Bosco Daudi na Mary Rameck wafugaji nyuki wao walisema kuwa vikwazo ni vingi
wanavyokabiliana navyo hususa ukusefu wa mitaji ya kununulia vitendea kazi hali
inayopelekea kutopata mavuno yenye tija na kujikuta wanadidimia kiuchimi
wakieleza kuwa wanakosa sifa za kukopa sababu wengi upande wajijini hawana hati
miliki za mali zao zinazotambulika
Katika mkutano huo, Bw Fales
Nzobona makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kibondo ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka
wafugaji hao na wakulima kufuata ushauri wanaopewa na wataalam ili waweze
kupata mazao yanayoridhisha licha ya kuwepo changamoto za mitaji midogo
Hata hivyo mkuu wa kitengo cha
maendeleo ya wafugaji nyuki katika halmashauri ya kibondo Seif Salum alisema wafugaji
wamekuwa wakikumbwa na shida ya kutokopesheka lakini hivi sasa kitengo chake
kinafanya utaratibu wa kuzijengea uwezo
taasisi na vikundi vya wafugaji
waungane kwa Bank haziwezi kumkopesha mtu mmojammoja
Nuhu Kaali Meneja wa Benki ya NMB
Tawi la Kibondo yeye alipoulizwa juu ya hali hiyo na mkakati gani unafanyika
anasema kuwa katika eneo lake anawashauri wakulima na wafugaji mbalimbali
kujiunga kwa pamoja na kusajili vikundi vya kwa mujibu wa utarati ili waweze
kuwa na kauli moja yenye nguvu ndipo wanapoweza kusaidiwa
Aidha Kaali amesema kuwa wao
wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi wilayani hapa,hivyo ni vema wakafuata
ushauri ili waweza kunufaika na kazi zao kwa kuwa hata serikali imekuwa
ikisisitiza wananchi kujiunga kwa pamoja
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni