HATARI: Wengi wanunua sabuni za dawa bila maelekezo ya wataalamu

Ni jambo lililozoeleka kwa sabuni zenye dawa kuuzwa mitaani, badala ya kwenye maduka maalumu. Uuzwaji huu wa kiholela usiozingatia afya ya mtumiaji unaweza kuwa na athari bila muhusika kufahamu.

Gazeti hili limebaini kuwa wengi wa wanaonunua sabuni hizo, kama Dettol, Rungu, Family na Life Bouy, hawanunui kwa ajili ya tiba badala yake hununua kulingana na zinavyonukia na zinavyotoa taka mwilini.
Endrew Mlungu, mkazi wa Buguruni Dar es Salaam, aliyekuwa akinunua sabuni hizo maeneo ya Buguruni

Chama, alisema kuwa anapenda kutumia Life Bouy kwa sababu akiogea zinamtakatisha na huziona taka zikimtoka wakati anajisugua.
Anasema pale hali yake ya kifedha inapokuwa si nzuri, hutumia sabuni nyingine lakini akiwa nazo anainunua kwa kuwa humuacha mwepesi na akioga, hufanya kweli.

“Nikiogea sabuni tofauti na hii najisikia kama sijaoga na hata nikiangalia sakafuni wakati najisugua sioni taka kwa maana hiyo hazitoi na hazinisafishi vizuri,” anasema Mlungu.
Mlungu anafafanua kuwa hafahamu kama ni dawa, na inawezekana kwa sababu ni dawa ndiyo maana akiogea inamtakasha, hivyo hana haja ya kusubiri kuandikiwa na daktari kwa kuwa zinapatikana kwa urahisi.

Sikujua Saidi mkazi wa Mbagala Dar es salaam, anasema kuwa anapenda kutumia sabuni ya Rungu kwa kuwa inanukia vizuri sio kama sabuni zinazopendwa kuwekwa kwenye  gesti za uswahili ambazo ukiogea kila mtu anakuhisi vibaya.

kuwa hata bei yake ni rahisi kwani akitoa Sh 1,000 anapata tatu, tofauti na sabuni nyingine huuzwa Sh 1500.
Richard Mwinyihija anasema kuwa hafahamu chochote kuhusu sabuni zipi dawa na zipi za kawaida anachoangalia ni ipi anaipata kwa ukaribu anapoihitaji.
Anafafanua kuwa anapohitaji sabuni huangalia bei na ataipata wapi, kama anapita njiani na kukuitana na sabuni hana haja ya kusubiri daktari amuandikie.
“Kama wao wangekuwa wanajua umuhimu wa sabuni hizi kutolewa kwa maelekezo ya daktari zingeuzwa kwenye maduka ya dawa, lakini zinauzwa huku kama zina madhara tutaumia wengi nani anajua kama ni dawa mimi mwenyewe na kukaa kwangu Mjini sijui, naona nikinunua hizi ndiyo kuelimika, ”anasema Mwinyihija.

Ustaadhi Salum anasema kuwa anashangaa kusikia kuwa hizo ni sabuni dawa kwani amekuwa akinunua kila anapozihitaji na mahali popote.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Matumizi ya simu kwa wanafunzi chanzo mmomonyoko wa maadili’

Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji