Kibondo;Chuo cha Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji
Alfrida Ndungulu mkuu wa chuo |
Atashasta Nditiye Mbunge jimbo la Muhambwe |
Kibondo;Chuo cha
Uuguzi kilichoko Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kina kabiliwa na matatizo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya majengo fedha kwa
ajili ya kuendeshea chuo hicho na ukosefu wa watumishi wakutosha hali inayopelekea kuathili ufundishaji
Chuo hicho hakina Jengo la Maabara kwa ajili ya kujifunzia
kwa vitendo kwa wanafunzi walimu waliopo ni watatu na mahitaji wanatakiwa wapo
walimu kumi na tano
Akiongelea swala hilo jana katika mahafali ya saba kwa wahitimu ngazi ya cheti mkuu wa chuo hicho
Alfreda Ndungulu alisema licha ya walimu kujituma kufanya kazi kwa bidii lakini
changamoto hizo zimekuwa zikiwalemea kwa kukosa mahitaji muhimu kama vifaa vya
maabara kwa ajili ya kufundishia huku akiiomba serikali kupitia wizara ya Afya maendeleo
ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto kulitazama kwa namna ya pekee
Nao wanafunzi waliokuwa wakihitimu kwenye chuo hicho cha
uuguzi ambao ni Adela James na Mary Esau, walisema ni vema serikali ikaweka mpango wa
kuwakopesha wanafunzi katika sekta ya
Afya kwa ni nayo ni muhimu huku
wakieleza hali waliyokuwa wakikumbana nayo wakati wa masomo yao walikuwa
wakitegemeaf edha kutoka kwa wazazi ambazo zilikuwa hazikidhi mahitaji na kulazimika kula mlo mmoja kwa sikua Adela
‘’Jinsi ambavyo mikopo inatolewa na serikali basin a sisi
tungewekewa utaratibu wa kupata mikopo kwa tunapata shida sana kwa kutegemea
fedha za wazazi ikilinganishwa hata huduma za afya ni muhimu kwani hata masomo
yake lazima uwe umetulia ili kupata uelewa mzuri wakati wa masomo bila kuwa
mawazo ya Ada na mahitaji mengine alisema Adela
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Atashaster Nditiye, ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali
hayo aliitaka jamii na wazazi wenye wanafunzi kuendelea kuchangia huduma za
elimu katika sekta ya Afya kwani
serikali bado inaendelea kulitazama kisera japo
ni muhimu kwani utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaopata elimu
katika Vyuo vya Afya hasa ngazi ya Cheti
haukuwepo ili kuondoa Nkanganyiko kwa sekta zingine
Laurian Kanaganwa Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya kibondo
yeye aliwataka wahitimu hao kutoridhika
na ngazi hiyo walinayo bali wajitahidi kujiendeleza zaidi kwakuwa mambo mengi
ya huduma za afya ya Binadamu yanabadilika kila kukicha
Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1977 kikiwakinatoa mafunzo
ya Mtoto kwa wakati huo, kilifungwa mwaka 1998 na kuanzishwa tena mwaka 2008 na
kuanza kutoa elimu ya Mafunzo ya Uuguzi ngazi ya Cheti na kwa mwaka huu wanafunzi walihitimu ni 45
tu
Maoni
Chapisha Maoni