Mkazi wa kijiji cha wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake
Mwemezi Muhingo Kibondo Mkazi wa kijiji cha Kumhama wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Peter Makala amemtaja mtu huyo kuwa ni Jaribu Obedi mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kumuhama wilayan kibondo Bw Makala amesema kuwa mnamo tarehe 28 mpaka 30 mwezi wa 5 mwaka huu majira ya usiku katika kijiji cha kumuhama bw Jaribu alimlawiti mkewe aitwae jina linahifadhiwa, mwenye umri wa miaka 24 akiwa na mimba ya miezi saba na kwamba alimfanyia kitendo hicho siku tatu mfurulizo Aidha kitendo hicho kilisababisha mishipa kukosa nguvu hali ambayo humsababishia kutoa haja zote mfululizo bila kujizuia wala kujitambua hali ambayo ilisababisha dada huyo kukosa uvumilivu na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi mtaa wa migombani mjini kibo...