Mkazi wa kijiji cha wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake
Mwemezi Muhingo Kibondo
Mkazi wa kijiji cha Kumhama wilayani kibondo mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatika katika kosa la kumlawiti mkewe kinyume na maumbile bila lidhaa yake
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kibondo bw Erick Marley mwendesha mashitaka wa polisi bw Peter Makala amemtaja mtu huyo kuwa ni Jaribu Obedi mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kumuhama wilayan kibondo
Bw Makala amesema kuwa mnamo tarehe 28 mpaka 30 mwezi wa 5 mwaka huu majira ya usiku katika kijiji cha kumuhama bw Jaribu alimlawiti mkewe aitwae jina linahifadhiwa, mwenye umri wa miaka 24 akiwa na mimba ya miezi saba na kwamba alimfanyia kitendo hicho siku tatu mfurulizo
Aidha kitendo hicho kilisababisha mishipa kukosa nguvu hali ambayo humsababishia kutoa haja zote mfululizo bila kujizuia wala kujitambua hali ambayo ilisababisha dada huyo kukosa uvumilivu na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi mtaa wa migombani mjini kibondo
Baada ya dada yake kupata taarifa hiyo alimpeleka muhanga huyo katika ofisi za ustawi wa jamii na kisha kupelekwa jeshi la polisi ambapo alipewa fomu namba tatu ili kwenda kutibiwa hospitalini ambapo uchunguzi wa madaktari ulionesha kuwa ni kweli amefanyiwa kitendo hicho
Kutokana na makossa hayo mahakama imemkuta na hatia bwana huyo na kumhukumu kifungo cha miaka 60 gerezani ili iwe fundisho kwake na watu wengine
Maoni
Chapisha Maoni