Serikali imeshauriwa kutengeneza utaratibu wa kuwatawanya Wakimbizi kwa kuanzisha makambi mengine zaidi katika mikoa mingine ili kuondoa mrundikano wa wakimbizi wengi katika eneo moja hatua inayosababisha kuwepo kwa uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali
Mwemezi Muhingo Kibondo
Serikali imeshauriwa kutengeneza utaratibu wa kuwatawanya Wakimbizi kwa kuanzisha makambi mengine zaidi katika mikoa mingine ili kuondoa mrundikano wa wakimbizi wengi katika eneo moja hatua inayosababisha kuwepo kwa uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali
Hayo yamesemwa na baadhi ya wadau wanaotoa huduma kwa wakimbizi katika wilaya za kakonko na kibondo mkoani Kigoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira Duniani yaliyohusisha na utoaji elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wakimbizi wa kambi ya Mtendeli wilayani Kakonko, kuwa ni vema makambi yakawa na idadi ndogo ya wakimbizi
Nyinisaheri Gwamagobe ambaye ni Maneja wa shirika lijulikanalo kama Relief Devolment Societ REDESO, linalohisika na utunzaji wa mazingira katika makambi ya wakimbizi amesema kuwa wakimbizi wanapokuwa wengi katika eneo moja husababisha uharifu mkubwa wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo mazingira kwa muda na kupungua uwezo wa kuwasimamia ipasavyo
Kwa upande wake Mratibu wa mazingira toka mambo ya Ndani kitengo cha wakimbizi Bw, Thobias Sijabaje amewataka wakimbizi wafuate maelekezo yanayotolewa na wataalam wa mazingira na watumie majiko yanayotumia kuni chache na kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi katika maeneo wanayoishi na kutojihusha na uwindaji haramu ikilinganishwa na kambi hiyo kuwa karibu na hifadhi ya wanyama pori ya Moyowosi Kigosi
Peter Toyma mkuu wa wilaya ya Kakonko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho yeye ameyetaka mashirika mbalimbali kuhakikisha yanafuatilia zoezi zima la utunzaji na uhifadhi wa mazingira linakuwa na tija simaneno tu bila utekelezaji huku mkuu wa kambi hiyo Inocent Mwaka, akiwataka wakimbizi kuacha kutorokea vijijini kwani nikinyume cha taratibu
Nao baadhi ya wakimbizi wamesema kuwa watajitahidi kuhakikisha wanatunza mazingira bila kukata miti hovyo japo kwao nishati inayotumika kupikia ni kuni na kudai kuwa kinachowafanya kutoroka makambini ni pale wanapoomba vibali na kunyimwa uamua kupitia njia za panya ili kutafuta vibarua waweze kupata mahitaji mengine
Maadhimisho hayo kwa wakimbizi yalikuwa na kauli mbiu isemayo tuhifadhi vyanzo vya majikwa uhai wa Taifa letu na tuache uwindaji haramu kwa faida ya kizazi cha sasa navijavyo
Maoni
Chapisha Maoni