Kakonko;Wakazi wa wilaya ya Kakokonko mkoani kigoma wamemuomba Mkuu wa wa mkoa huo Brigedia General Msitaafu, Emmanuel Maganga kusimamia vema vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo baada ya kuingiwa na hofu kutokana na matukio ya mauwaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara
Mwemezi Muhingo, Mwananchi
Add caption |
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedi General a Mstaafu Emmanuel Maganga wa tatu kutoka kulia akiwa amekaa kwenye madawati baada ya kukabidhiwa toka kwa meneja wa NMB kanda ya magharibi mjini Kakonko |
Kakonko;Wakazi wa wilaya ya Kakokonko
mkoani kigoma wamemuomba Mkuu wa wa mkoa huo Brigedia General Msitaafu,
Emmanuel Maganga kusimamia vema vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo
baada ya kuingiwa na hofu kutokana na matukio ya mauwaji ambayo yamekuwa
yakijitokeza mara kwa mara
Vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikifanyika katika maeneo
mengi wilayani humo, watu wananyang’anywa mali zao wanajeruhiwa na wengine
kuuwawa kikatili kwa kupigwa risasi na watu ambao wamekuwa hawafahamiki huku
vyombo vya ulinzi vikidai vinaendelea na uchunguzi bila kutoa maelezo
yanayoeleweka kwa wananchi
Wakiongea jana katika kikao kilicho wahusisha viongozi
wadini, madiwani watendaji kata na vijiji na wakuu wa Idara na kamati za ulinzi
na usalama wilayani humo, mmoja wa wakazi hao Bw, Ismail Ntoteye alimwambia
mkuu wa Mkoa huo kwa watu wamekuwa wakishambuliwa na kunyang’anywa vitu ambavyo
wakati mwingine havina hata thamani yoyote kama simu za mkononi za kawaida na
pesa ndogondogo
‘’Tunashindwa kuelewa uvamizi huu unaofanyika mapema kabisa
uenda unafanywa vikundi vya uharifu kutoka nchi jirani kwa kuwa tuko mpakani na
kila tunapo lieleza Jeshi la Polisi utueleza kuwa tunaendelea na uchunguzi na
hatujui kama watu hao wanakatwa na
baadae tunasikia watu wengine wamevamiwa hali hii inatusababishia hofu kubwa
alisema Ntoteye’’
Kwa upande wake Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma Brigedia General
msitaafu, Emmanuel Maganga alisema kuwa swala hilo atalifanyia kazi lakini
kinachotakiwa ni wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi kwani watu
wengi hawajitokezi kuoa maelezo hata kama wanmfahamu mwalifu
Aidha Magnga aliwaeleza wajumbe wakikao hicho kuwa waache
kutoa visingizio vya kuwa wanaowavamia ni watu wanovuka mipaka kutoka nchi
jirani kwa kusema kuwa hata waalifu wanakuwemo miongoni mwao watanzania wenyewe
na hawataki kuwafichua ili wahojiwe na
kama watabainika hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya
Pamoja na mambo mengine Mkuu hyo wa mkoa aliwataka viongozi
wa vijiji na watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanashirikiana na wanachi
katika kazi za maendeleo kwa kuacha kuficha mambo ambayo yanaihusu jamii hali
inayopelekea manung’uniko mara kunapotokea kukwama kwa shuguli hizo
Maganga alikazia juu ya Pesa zilizoahidiwa na serikali kuwa
itatoa tsh milion 50 kila kijiji akiwataka kuhakikisha wanwaelewesha
wananchi wajiunge katika vikundi na
hakuna kuzitumia kwa mambo mengine bali ni kwa ajili ya kuinua uchumi wa
wananchi huku akisema kuwa maali pengine viongozi wa halmashauri ukiuka
taratibu wanazopewa na kuamua kutengeneza vikundi vyao ili waweze kufanya
ubadhilifu wa pesa za walengwa. Na kusema atakaebainika atachuliwa hatua za
kisheria
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni