Mkuu wa mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amewataka watumishi wa Serikali kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea pamoja na kutafuta maslahi binafsi pasipo kuihudumia jamii kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma hali inayo sababisha malalamiko kwa wananchiMkuu wa mkoa wa Bligedia General Emmanuel Maganga alipokuwa akizungumza na wakazi wa kifura alipotembelea kituo cha afya na kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga
Mkuu wa mkoa wa kigoma Emmanuel Maganga akiongea na wakazi wa kifura alioweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha afya kushoto Ruth Msafiri Mkuu wa wilaya ya kibondo |
Mkuu wa mkoa wakigoma Emmanuel Maganga akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga kituo cha afya kifura |
Mkuu wa mkoa wa Kigoma
Emmanuel Maganga amewataka watumishi wa
Serikali kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea pamoja na kutafuta
maslahi binafsi pasipo kuihudumia jamii kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa
umma hali inayo sababisha malalamiko kwa wananchi
Kauli hiyo ametoa
jana wakati akizungumza na wakuu
wa Idara za halmashauri na serikali kuu mjini kibondo mkoani humo,
katika ziara yake ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa
kigoma akisisitiza kuwa,hali hiyo ndiyo inayopelekea kuwepo kwa mianya ya
rushwa na ubadhilifu wa mali za serikali
Alisema kuwa wapo watumishi wa serikali wasiyokuwa waadilifu
na wasijali kazi zao na kutimiza wajibu wao
kwa kutumia taaluma zao huku wakitafuta faida zao wenyewe bila kujali
wananchi vitendo ambavyo havikubali kwani vinasababisha usumbufu usiyokuwa wa
lazima kwa wananchi
‘’Kila mtu akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu na
miongo ya utumishi wa umma hakuna sababu ya wananchi kulailalamikia serikali
hadi kuta kufanya maandamano na anayeona hawezi kufuta taratibu za kazi kwa
kuwatumikia wananchi ajiondoe mapema kuliko kuendelea kuvuluga alisema
Maganga’’
Katika ziara hiyo aliweza kutembelea baadhi ya miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa kuwashirikisha wananchi ambapo alikagua utengenezaji wa
madawati na ukarabati wa vyumba vya madarasa na kujionea hali ngumu ya ukosefu
wa vyoo katika shule ya msingi Kumhama na Shunga na kuwataka walimu kutumia
vizuri pesa wanazotolewa na serikali
Aidha Mkuu huyo wa mkoa wa kigoma alitembelea kituo cha Afya
kifura na kuweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa nyumba ya kuishi watumishi wa
afya, nakukagua jengo la upasuaji lililokwishaanza kazi yake na kuwataka wananchi kulinda kutunza
mali za umma na kuthamini misaada inayotolewa na mashirika mbalimbali kupitia
serikalini
Maoni
Chapisha Maoni