Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.
Moja ya malori yaliyoteketezwa Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano. Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika Licha ya majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo. Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa misaada kufuatia shambulio hilo. Mjumbe ...