Maafisa wa jeshi la ulinzi wa rais wamehusika katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama cha upinzani, watu wawili waliojeruhiwa wameambia BBC.
Add caption |
Maafisa wa jeshi la ulinzi wa rais wamehusika katika shambulio dhidi ya makao makuu ya chama cha upinzani, watu wawili waliojeruhiwa wameambia BBC.
Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo yaliteketezwa moto katika mashambulio ya usiku kwenye mji mkuu Kinshasa.
Kumekuwa na miili ya watu wawili ilioteketezwa moto katika ofisi hizo zilizoharibiwa za muungano mkuu wa upinzani DRC (UDPS).
Msemaji wa jeshi la Congo ameiambia BBC hana la kusema kuhusu shutuma hizo.
Upinzani unasema zaidi ya watu 50 wameuawa Jumatatu wakati wa maandamano kumpinga rais Joseph Kabila.
Serikali inasema idadi ya waliouawa ni watu 17.
Vikosi vya usalama vimeshutumiwa kwa kutumia risasi dhidi ya waandamanaj hao wa amani waliotaka kutolewa tarehe ya uchaguzi wa urais nchini.
Maoni
Chapisha Maoni